MH370 ndege ya Malaysia iliyopotea ikiwa njiani kutoka
Malaysia kuelekea China
Serikali ya Malaysia imesitisha shughuli ya kuitafuta ndege
ya iliyopotea ya MH370 na kuitaja kama ajali huku ikisema hapakuwa na manusura
wa ajali hio.
Hapajawi kuoenekana dalili ya ndege hiyo iliyopotea ikiwa
safarini kuelekea China kutoka Malaysia tarehe 8 mwezi Machi mwaka 2014,
Maafisa wakuu wanasema shughuli ya kuipata ndege
hiyo, bado
inaendelea lakini inasemekana abiria 239 waliokuwa kwenye ndege hio walifariki.
Ndege hiyo bado haijulikani iliko na wala kujulikana
ilikopotelea licha ya shughuli kubwa ya kimataifa kuitafuta ksuini mwa bara
hindi.
Tangazo la serikali ya Malaysia, Alhamisi, inatoa fursa kwa
jamaa wa waathiriwa wa ajali hio kulipwa fidia.
Maafisa waliongeza kusema kwamba serikali bado imeipa
kipaombele shughuli ya kuitafuta ndege hio na kwamba imefanya kila iwezalo
angalu kupata dalili ya ikokwenda.
Vyombo vinne vya baharini vilivyokuwa vinafanya msako
baharini kwa kutumia teknolojia ya kisasa 'Sonar' kutafuta angalau mabaki ya
ndege hio vimesitisha shughuli hio.
Kulingana na picha za Satelite, mabaki ya ndege hiyo huenda
yako katika ufuo wa mji wa Perth Magharibi mwa Australia.
No comments:
Post a Comment