Pages

Saturday, January 17, 2015

MWILI WA DEREVA BW ALLI ATHUMANI ALLI UMEKUTWA UKIWA UMENYONGWA NDANI YA GARI ALILOKUWA ANAENDESHA.


Mwili wa aliye kuwa dereva wa gari la mizigo Bw Alli Athumani Alli ambaye alikuwa akitafutwa na jeshi la Polisi kufuatia wizi wa milango umekutwa ndani ya gari alilokuwa anaendesha baada ya siku 4 ukiwa umenyongwa na kamba za kubebea mizigo mikubwa huku gari hilo likiwa limeegeshwa kituoni hapo.

Akizungumzia na ITV kamanda wa polisi mkoa wa Ilala kamishina msaidi mwandamizi wa polisi Mary Nzuki amekili kutokea kwa tukio hilo ambapo baada ya watu hao kufanya mauaji hayo waliuweka mwili huo katika kitanda kilichopo katika gari hilo na kuiba mzigo wa milango uliokuwepo katika gari hilo ambao ulikuwa ukitokea bandalini kwenda katika ghara la mizigo la kampuni ya J Fogh Logistics.
Aidha katika hatua nyingine kamanda Nzuki amesema baadhi ya milango imekwisha patikana na jumla ya watu saba wamekamatwa kuhusiana na tukio hilo ambapo watu hao watafikishwa mahakama pindi uchunguzi utakapo kamilika.



Akizungumzia tukio hilo dereva mwezake na marehemu Bw Sultani Salum ambaye alifika kituoni hapo kwa ajili ya kuchukua gari hilo amesema kuwa yeye ndiye aliye gundua kuwepo kwa mwili huo baada ya kuona damu ikitokea kitandani na hivyo kulazimika kutoa taarifa ya kuwepo kwa tukio hilo.

CHANZO: ITV TANZANIA

No comments:

Post a Comment