Japan Hostages
Rais wa Marekani Barack Obama amelaani kile alichokitaja
kuwa mauaji ya kikatili ya mmoja wa raia wa Japan aliyekuwa akishikiliwa mateka
na wanamgambo wa Islamic State Haruna Yukawa.
Rais Obama pia alitaka mateka mwingine anayeshikiliwa na
wanamgambo hao mwandishi wa habari Kenji Goto kuachiliwa mara moja
Kwa njia ya video Goto alionekana kwenye mitandao akishika
mkononi picha ya maiti ya bwan Yukawa.
Mapema wataalamu mjini Tokyo na Marekani walisema kuwa
wanatathmini ukweli wa picha hiyo.
Waziri mkuu nchini Japan Shinzo Abe alisema kuwa
ameghadhabishwa na video hiyo.
No comments:
Post a Comment