Dar es Salaam. Vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi
(Ukawa) vimetangaza rasmi kutoshiriki katika mchakato wa kura ya maoni
ya katiba na kwamba kuanzia sasa vitahamasisha wananchi kuunga mkono.
Uamuzi huo umetolewa leo na wenyeviti wa vyama
wanaounda umoja huo wa ukawa ambao ni Mwenyekiti wa Chadema, Freeman
Mbowe, Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba, Mwenyekiti wa
NCCR-Mageuzi, James Mbatia na Mwenyekiti wa NLD, Makaidi.
Akizungumza wakati wa kutoa msimamo huo Profesa
Lipumba amesema wamefikia uamuzi wa kutoshiriki katika zoezi hilo kwa
sababu mchakato mzima haukuwa na maridhiano ya kitaifa.
“Vyama vya siasa ikiwemo CCM vilikubaliana mwaka
jana kwamba zoezi la kura za maoni lifanyike mwaka 2016 baada ya
uchaguzi mkuu, tulisaini wote na Rais Jakaya Kikwete alikubali, kwa nini
mabadiliko yafanyike ghafla” amehoji Profesa Lipumba.
Amesema jambo la kushangaza, Rais Kikwete aligeuka
na kutangaza kwamba Aprili 30, mwaka huu kuwa siku ya kupiga kura ya
maoni kuhusu Katiba Mpya.
Amesema pamoja na kutangaza siku ya kupiga kura,
bado uandikishaji katika daftari la wapiga kura haujaanza kwa sababu
wanasubiri vifaa.
“Hadi sasa vifaa vya Biometric Voter Registration
(BVR) vilivyopo ni seti 250 wakati vinavyohitajika ni seti 7500, tume
inasubiri hadi sasa, zoezi hili litafanyika kweli?,” alihoji Lipumba.
“Mbinu hiyo inafanywa na Serikali kwa sababu Wazanzibari ndiyo wanaona kikwazo kwao,” alisema Makaidi.
Aprili 16 mwaka jana, Wabunge wa Bunge Maalum la
Katiba kutoka vyama vya Chadema, CUF, NCCR-Mageuzi na NLD walitoka nje
wakidai bunge hilo lilikuwa halijadili maoni ya wananchi
yaliyowasilishwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba.

No comments:
Post a Comment