Kwa mujibu wa mtandao wa MySanAntonio.com,Eleby aliahidi
kwamba ikiwa hatapata mchumba wakati atakapokuwa ametimiza miaka 40, basi
atafanya harusi ya mtu mmoja yaani atajioa ili kusherehekea miaka yake 40.
Duru zinasema kuwa mwanamke Eleby alifanya harusi yake
mwenyewe katika makavazi ya Houston akiambatana na jamaa na familia yake na
wageni wengine waalikwa.
Kwa sherehe hii, dadake Eleby ndiye aliendesha sherehe hio,
kwani ni kinyume na sheria kwa mtu kujioa mwenyewe. Harusi ya kawaida ni kati
ya watu wawili.
Katika picha za kanisani sherehe ilionekana kuwa ya kawaida
bila ya mchumba.
Kulingana na John Guess Jr afisaa mkuu wa makavazi hayo,
sherehe hiyo ilionekana kuwa bila tashwishi na kuonekana kama jambo la kawaida
kwani makavazi hayo huwakumbatia watu wa jinsia mbali mbali kuendesha harusi
zao hapo.
Aliposikia kwamba Eleby, ambaye anaishi na kufanya kazi
ugenini alikuwa anapanga kujioa mwenyewe, aliharakisha kwenda katika eneo hilo
kujionea mwenyewe.
"Eleby alipofikisha umri wa miaka 40 bila ya kupata
mpenzi na mtu mwenye nia ya kumuoa, aliamua angejioa mwenyewe,''alisema Guess
Jr ambaye anasema harusi hiyo imewashangaza wengi na kuwa gumzo katika mitandao
ya kijamii.
Anasema anakubaliana na Eleby na mtazamo wake wa mapenzi
kwamba mtu anaweza kujipenda na kujioa kwa kukosa wa kumuoa kwani cha muhimu ni
mtu kujipenda kwanza kabla ya kupendwa.
"watu wengu huolewa bila ya kutafakari mara mbili
kuhusu yule anayemuoa, '' Guess Jr alisema.
Anadhani kwamba pindi watu watakapomuona Eleby
anavyojishughulikia mwenyewe, huenda akapata ushindani.
"ni mrembo, anafanya kazi kwa bidii na anasifika
duniani na pia anaona uamuzi wake umewapa gumzo watu wengi. ''
No comments:
Post a Comment