Wakizungumzia tukio hilo linalodhaniwa kutokea kuanzia asubuhi ya Januari 25,2015, hadi majirani walipogundua tukio hilo usiku jana, Mwenyekiti wa Mtaa wa Barehani pamoja na wananchi walioshuhudia tukio hilo wanasema kuwa mchana watoto hao hawakuonekana kama mazoea yao ambapo wamekuwa wakionekana kila siku nyakati za mchana wakicheza.
Jeshi la Polisi mkoani Tabora limethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuwataja marehemu kwa majina ya Mwamvua Mrisho (4) na Soud, (miezi 4) na upelelezi unaendelea pindi utakapokamilika mtuhumiwa atafikishwa Mahakamani.
Chanzo cha tukio hilo bado hakijajulikana na mtuhumiwa yuko mikononi mwa polisi hadi sasa.
No comments:
Post a Comment