KATIKA hali ya kushangaza, polisi walijikuta wakipata
shughuli pevu kumkamata staa asiyeishiwa matukio Bongo, Wema Sepetu ambaye
alidaiwa kupiga muziki kwa sauti kubwa usiku kucha pasipo kuwa na kibali, Amani
linakupa mchapo.
Timu iliyofika nyumbani kwa Wema Sepetu kumkamta kwa
usumbufu aliosababisha kwa majirani.
“Kwa kweli ni kero, kila mara amekuwa na tabia ya kupiga
muziki mkubwa katika sherehe zake ambazo hazina kichwa wala miguu. Kama jana
(usiku wa Jumatatu) muziki ulifunguliwa kuanzia saa mbili usiku mpaka asubuhi
na majirani walimfuata Wema mara kadhaa kumtaka apunguze sauti lakini aliwajibu
vibaya.
Polisi akisimamia zoezi hilo kwa kuwawajibisha wahusika (mmiliki wa muziki na mwenye sherehe).
Mapaparazi wetu walichukua usafiri wa pikipiki na kuwahi
fasta na kukuta polisi wakihangaika kwa muda mrefu kumkamata mrembo huyo lakini
ikashindikana kwa kuwa alikuwa amelewa na kukimbia hovyo huku akiwa nusu utupu.
Mwenye sherehe, Neema( rafiki wa Wema Sepetu) akichukuliwa
kwenye bajaji.
“Kwa sababu hiyo walimkamata mmiliki wa muziki ambaye jina
lake halikupatikana mara moja na mwenye sherehe (Neema) kisha kwenda nao katika
ofisi za mtendaji, Kijitonyama kwa ajili
ya hatua za kisheria,” alisema.
Msanii wa filamu Bongo, Wema Sepetu.
Akizungumza na gazeti hili, mwenyekiti wa mtaa huo, Mzee
Haogwa, alithibitisha kuletewa malalamiko ya Wema na kufika nyumbani hapo
ambapo pia alidai alishangazwa na kitendo cha kuwakuta wanaume tata kwenye
sherehe hiyo.
No comments:
Post a Comment