Ronaldo de Lima anavyoonekana sasa.
Mshambuliaji wa zamani wa timu ya taifa ya brazil Ronaldo
Luís Nazário de Lima anatarajia kurejea tena dimbani.
De lima ameahidi kupunguza mwili wake kwa mazoezi kwa lengo
la kurejea uwanjani kukipiga na timu Fort Lauderdale inayocheza ligi daraja la
pili nchi Marekani.
Akizungumza na waandishi wa habari Ronaldo
mwenye miaka 38
amesema "kucheza soka lazima uwe na mwili mzuri wa nitajaribu ni
changamoto nina uhakika nitaisaidia ligi na timu."
Ronaldo alitwaa ubigwa wa kombe la dunia mara mbili mwaka
1994 na 2002 akiwa na kikosi cha Brazil.
Amewahi kuvitumikia vilabu vya Barcelona, PSV Eindhoven,
Inter Milan and Real Madrid kwa mafanikio makubwa sana.
No comments:
Post a Comment