Baada ya masaibu ya kujitakia urembo bandia, Urach hawezi tena
kutembea kwani kwa sasa anatumia kiti cha magurudumu
|
Andressa Urach alimaliza wa pili katika mashindano ya urembo
ambapo mashabiki walimpigia mwanamke waliyehisi kuwa na makalio mazuri zaidi
katika nchi yao kupitia kwenye mtandao wa internet.
Ili kujiongeza urembo, Urach aliambia jarida la Daily Mail
la Uingereza kwamba alidungwa sindano za kemikali ili kufanya makalio yake kuwa
makubwa pamoja na kuongeza ukubwa wa miguu yake.
Lakini mnamo mwaka 2013, mwili wake ulianza kuoza ndani.
Athari za kujiweka urembo bandia zilianza kumwandama wakati
Urachhadi madaktari wakalazimika kutoa kemikali hizo kutoka mwilini mwake mwezi
Novemba kwa kuchimba mashimo katika mapaja yake.
Mwili wake ilipatwa na mshtuko kwa sababu ya ugonjwa
alioupata kwa kutumia vifaa chafu vya matibabu mwilini mwake.
Madaktari wametoa kemikali za sumu mwilini mwa Urach
|
Madaktari hata hivyo waliweza kuokoa maisha yake lakini hadi
leo anatumia tu kiti cha magurudumu na miguu yake ina mashimo mwengi ambayo
madaktari waliweza kutoboa ili kutoa kemikali zenye sumu alizotumia kuongeza
ukubwa wa makalio na miguu.
''Ninalipia makosa yangu leo kwa sababu nilitaka urembo kwa
kila hali, ili nionekane kuwa kamili. Mungu ananiadhibu'' Urach aliambia Mail.
''Lakini badala ya kujiongeza urembo, niliharibu mwili wangu
na sasa hata hauna sura.''
Urach anasema Mungu alimpiga kiboko kwa kujaribu
kujibadilisha mwili wake kwa sababu ya kujitakia umaarufu
|
Urach pia alisema kwamba alikuwa na mazoea mabaya ya
kufanyiwa uapasuaji wa kujiongeza urembo bandia kila alipojihisi kufanya hivyo.
''Sikuwahi kutafakari mara mbili wakati nilipokuwa nafanyiwa
upasuaji lakini watu waliponionya nilidhani tu nitaweza kukabiliana na athari
za hayo baadaye. '' Ningeweza kwenda kwa daktari, kama mfano nilivyozoea kwenda
dukani na kuchagua nilichokitaka. Nilitaka watu wanitazame na kusema tu ,
''wow''
Kwa sasa Urach amejitwika mzigo wa kuwatahadharisha wanawake
wengine kuhusu hatari za urembo bandia.chanzo bbc
No comments:
Post a Comment