Wiki iliyopita tuliweza kuona nini maana kubwa ya tatizo
hili la kutokwa na kijinyama katika sehemu au maeneo ya haja kubwa na leo
tutaweza kuona basi vyanzo au visababishi hasa vya tatizo hili kwa mwanadamu.
VISABABISHI
Sasa wataalamu bado hawajawa na majibu kamili kuhusiana na
tatizo hili la kutokwa na kijinyama katika maeneo ya haja kubwa husababishwa na
kitu gani hasa lakini wameweza kutoa baadhi ya vitu ambavyo vinaaminika kwa
kiwango kikubwa sana husababisha hali hii kujitokeza kwa mwanadamu, na vitu
hivyo basi ni kama vifuatayo;
Kupata choo kigumu kupita kiasi kwa mwanadamu wataalamu
wanaita constipation mara nyingi imekuwa ni chanzo kikubwa sana cha tatizo hili
la mtu kutokwa na kinyama katika maeneo ya haja kubwa na kuna uwezekano ikawa
ni bawasili ya ndani au ya nje yenye kuonekana, kwa hiyo kama mtu anakumbwa na
hali ya kupata choo kigumu basi
kunauwezekano mkubwa sana mtu huyo akasumbuliwa
na tatizo hili la bawasili.
Hali ya kuharisha sana {heavy diarrhea}, kwa mtu ambaye
anapatwa na hali ya kuharisha kwa muda mrefu basi naye pia anauwezekano mkubwa
sana wa kukumbwa na tatizo hili la kutokwa na kijinyama katika maeneo ya haja
kubwa au bawasili {hemorrhoid}.
Kukosekana kwa baadhi ya vyakula, kuna baadhi ya vyakula
vinapokosekana katika mwili wa mwanadamu au visipotumika sana kwa mtu huweza
kusababisha mtu kupata choo
kigumu kupita kiasi na kama anapatwa na hali hii basi
kunauwezekano mkubwa sana mtu huyo akakumbwa na tatizo la bawasili na vyakula
hivyo ni mboga za majani na matunda kwa wingi ndani ya mwili.
Hali ya ujauzito kwa akina mama, hii pia imekuwa ni sababu
kubwa sana inayosababisha suala zima la kutokwa na kijinyama maeneo ya haja
kubwa na hii ni kwa sababu hali ya ujauzito kwa mama husababisha kukua au
kuongezeka kwa mji wa mimba ambao hutumika hasa kumuhifadhi mtoto na kwa sababu
hii basi inaweza kusababisha vascular structure au vijinyama katika maeneo ya
haja kubwa kwa mama kuongezeka ukubwa na hivyo basi kuwa ni tatizo,
lakini mara nyingi mwanamke akishajifungua kunauwezekano
kikapotea lakini kama kinabaki basi ni vema kufika katika vituo vya afya kwa
ajili ya matibabu zaidi.Kukaa kwa muda mrefu, hali ya kukaa kwa muda mrefu kwa
mwanadamu nayo pia imekuwa ni kisababishi kikubwa sana cha tatizo kubwa la
tumbo kujaa gesi na kupata choo kigumu kupita kiasi {constipation}.
Mara nyingi watu wanaokumbwa na shida hii kunauwezekano
mkubwa sana wa kutokwa na kinyama au bawasili, hasa kwa wanaotumia sana vyoo
vya kukaa na kufanya hivyo kwa muda mrefu.
Hali ya wanadamu kunyanyua vitu vizito kupita kiasi kwa
mwanadamu na ikawa ni zoezi endelevu kwa muda basi hali hii inaweza sababisha
mtu kupatwa na tatizo la kutokwa na kijinyama au bawasili.
Itaendelea wiki ijayo.
, na hata kwa mtu anaefanya kazi mgumu sana pia
kunauwezekano akakutwa na tatizo hili.
Na pia kunasababu ya kurithi, hali hii ya ya kutokwa na
kijinyama kwa upande mwingine wataalamu wametoa sababu ya kwamba inakua ni hali
ya kurithi kutoka kizazi kimoja kwenda kizazi kingine {genetic}, na ni vema kulitibia
pale tu linapojitokeza.
Na kama unapatwa na hali kama hiyo basi na wewe pia unaweza
wasiliana nasi kupitia namba zetu kwa ajili ya ushauri na tiba zaidi. Kwa
ushauri, vipimo na tiba dokta anapatikana kwenye vituo vyake vya Dar es Salaam,
Tanga, Morogoro na Mwanza.Nawatakia afya iliyo njema kabisa.
Itaendelea wiki ijayo. Asante.NA GPL
No comments:
Post a Comment