Picha za mabaki ya ndege ya AirAsia yaliyowekwa na Waziri wa Ulinzi wa Singapore, Ng Eng Hen kwenye ukurasa wake wa Facebook leo. SEHEMU kubwa ya mabaki ya ndege ya AirAsia QZ8501 iliyoanguka baharini ikiwa na watu 162 mwaka jana yameonekana na kupigwa picha katika Bahari ya Java.
Mkuu wa Mamlaka ya Uokoaji na utafutaji Indonesia, Bambang Soelistyo, amesema mabaki hayo yameonekana jana, Jumanne.
Waziri wa Ulinzi wa Singapore, Ng Eng Hen, leo ameweka picha za ndege hiyo katika ukurasa wake wa Facebook na kuandika kuwa picha hizo zinathibitisha kuwa ndege iliyoanguka baharini ni AirAsia QZ8501.
AirAsia ilipoteza mawasiliano na waongoza ndege Desemba 28,mwaka jana ilipokuwa ikitokea Surabaya nchini Indonesia kuelekea Singapore ikiwa na jumla ya watu 162.
Miili 40 tayari imepatikana kutoka Bahari ya Java ila wengi wa watu waliokuwa kwenye ndege hiyo wanadaiwa kuwa bado wamekwama ndani.
Mpaka sasa vifaa viwili vya kutunza kumbukumbu za ndege (black boxes) na mkiwa wa ndege hiyo vimepatikana na kupelekwa sehemu husika.
No comments:
Post a Comment