Mahakama nchini Misri imetoa hukumu ya kifungo cha maisha
dhidi ya Watu 230 akiwemo mmoja kati ya Wanaharakati vinara walioongoza
harakati za kuuangusha utawala wa Hosni Mubarak kwa makosa ya kushiriki katika
maandamano dhidi ya Serikali ya Cairo miaka mitatu iliyopita.
Mwanaharakati Ahmed Douma pia ametozwa faii ya Dola milioni
2.2 kwa kosa la kuchoma moto taasisi ya mafunzo ya Sayansi.
Kesi hiyo ilihusishwa na mapigano nje ya majengo ya wizara
jijini Cairo mwezi Desemba mwaka 2011.
Miongoni mwa mashtaka yanayomkabili ni pamoja na
kuwashambulia Maafisa usalama na kuvamia ndani ya Jengo la Wizara ya mambo ya
ndani.
Kwa kosa hilo Douma kwa sasa anatumikia kifungo cha miaka
mitatu.
No comments:
Post a Comment