Aliyekuwa rais wa Zambia Kenneth Kaunda amelazwa hospitalini
Aliyekuwa rais wa Zambia Kenneth Kaunda amelazwa hospitalini
mjini Lusaka.
Rais mpya wa taifa hilo Edgar Lungu amemtembelea kiongozi
huyo wa zamani mwenye umri wa miaka 90 hospitalini.
Kaunda aliliongoza taifa hilo kwa miaka 27 tangu lijipatie
uhuru wake mwaka 1964.
Alikuwa mwenyeji wa makundi mengi ya kupigania uhuru na
usawa wa watu weusi wakati wake.
Licha ya kuwa kiongozi maarufu,alikashifiwa kwa uongozi wake
wa kutumia mabavu.
Lakini Kaunda alikubali kuwacha mamlaka katika uchaguzi wa
kwanza wa vyama vingi mwaka 1991.
No comments:
Post a Comment