Wapiganaji wa islamic state
Zaidi ya watu millioni moja katika mtandao wa facebook
wameiona video katika mtandao kuhusu ajuza moja kutoka Syria anayewakashifu
wapiganaji wawili wa kiislamu akiwaambia ''rudini kwa mungu'' .
Mwanamke huyo aliwakaripia wanaume wawili ambao walikuwa
wakichukua kanda hiyo ya video.
''Musiwachinje wenzenu nao pia hawafai kuwachinja''...ni
haram...kati yenu na rais Bashar al Asaad hakuna atakayeshinda''.
Hatahivyo watu hao wawili walimjibu wakisema hawana muda wa
kupoteza naye ila tu anawafurahisha.
Na baadaye bibi huyo anaonekana akiwaita 'punda',na watu hao
wanaonekana wakicheka.
Kanda hiyo ya Video iliwekwa katika mtandao wa facebook na
Bint Jbeil,raia wa kusini mwa Lebanon mwenye mtandao ulio maarufu kwa watu wa
madhehebu ya kishia.
Mtandao ulidai kwamba ni mama mzee aliyekuwa akiwakosoa
wapiganaji wa IS.
No comments:
Post a Comment