Kamanda Mwaruanda
MWANAMKE mmoja Clemencia Nowa (50) anashikiliwa na polisi
baada ya kumpiga kichwa mume wake na
kumsababishia umauti. wanandoa hao ni wakazi wa kijijini cha Miangalua wilayani Sumbawanga koani Rukwa.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa , Jacob Mwaruanda alimtaja mume aliyekufa kuwa ni Stephen
Shauri (72) na kusema mkasa huo ulitokea
alfajiri ya Februari 04, mwaka
huu nyumbani kwao.
Akisimulia mkasa huo , Mwaruanda alieleza kuwa mara kwa mara majirani walimsikia akimshutumu mume kuisaliti ndoa yao lakini mume amekuwa akikana kutokuwa na
mwanamke mwingine nje ya ndoa yao .
Inadaiwa asubuhi hiyo
Clemencia alimkwida mumewe
na kumtandika kichwa cha nguvu
kilichosababisha aanguke na kufa papo
hapo .
Kwamujibu wa Kamanda Mwaruanda mtuhumiwa huyo alikamatwa namajirani zake ambao walimfikisha katika Kituo cha Polisi Laela
.
Source:Mchangiaji Rukwa
|
No comments:
Post a Comment