Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Friday, February 20, 2015

Chadema yavuta kasi mbio za urais Zanzibar


Dar/Zanzibar. Wakati NCCR-Mageuzi na CUF wakitangaza nia ya kugombea urais wa Zanzibar, Chadema bado wanaangalia mvumo wa upepo kabla ya vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) kuteua mwakilishi mmoja wa kupambana na CCM.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Seif Sharrif Hamad, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa CUF, ameshatangaza kujitosa kuwania nafasi hiyo, sambamba na Mwenyekiti wa NCCR wa Zanzibar, 



Ambari Khamis Haji.
Naibu Katibu Mkuu wa Chadema (Zanzibar), Salum Mwalimu alisema maandalizi ya ndani ya chama yanaendelea, huku pia vikao binafsi vya chama na kile cha Ukawa navyo vikifanyika kwa lengo la kupitisha jina la mgombea mmoja.
CUF na NCCR Mageuzi
Kujitokeza kwa Ambari, aliyegombea nafasi hiyo uchaguzi uliopita, kutaleta ushindani mkubwa ndani ya Ukawa na Maalim Seif.
Ambari alisema uamuzi wake wa kuwania nafasi hiyo umetokana na uwezo wake na kukubalika na wananchi na sera za NCCR-Mageuzi kuwa makini.
“Hii ni haki yangu kikatiba, kiraia na kidemokrasia. Naamini chama changu kitanipa baraka zote kufanikisha jambo hili. Uamuzi wangu haulengi kusaliti Ukawa,” alisema.
Alisema Zanzibar kulingana na historia yake inahitaji kupata mabadilko ya kiutawala na kisera kutokana na wananchi wengi kuchoshwa na sera za CCM.

No comments:

Post a Comment