Dar/Zanzibar. Wakati NCCR-Mageuzi na CUF wakitangaza nia ya
kugombea urais wa Zanzibar, Chadema bado wanaangalia mvumo wa upepo
kabla ya vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) kuteua
mwakilishi mmoja wa kupambana na CCM.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Seif Sharrif
Hamad, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa CUF, ameshatangaza kujitosa kuwania
nafasi hiyo, sambamba na Mwenyekiti wa NCCR wa Zanzibar,
Ambari Khamis Haji.
Ambari Khamis Haji.
Naibu Katibu Mkuu wa Chadema (Zanzibar), Salum
Mwalimu alisema maandalizi ya ndani ya chama yanaendelea, huku pia vikao
binafsi vya chama na kile cha Ukawa navyo vikifanyika kwa lengo la
kupitisha jina la mgombea mmoja.
CUF na NCCR Mageuzi
Kujitokeza kwa Ambari, aliyegombea nafasi hiyo uchaguzi uliopita, kutaleta ushindani mkubwa ndani ya Ukawa na Maalim Seif.
Ambari alisema uamuzi wake wa kuwania nafasi hiyo
umetokana na uwezo wake na kukubalika na wananchi na sera za
NCCR-Mageuzi kuwa makini.
“Hii ni haki yangu kikatiba, kiraia na
kidemokrasia. Naamini chama changu kitanipa baraka zote kufanikisha
jambo hili. Uamuzi wangu haulengi kusaliti Ukawa,” alisema.
Alisema Zanzibar kulingana na historia yake
inahitaji kupata mabadilko ya kiutawala na kisera kutokana na wananchi
wengi kuchoshwa na sera za CCM.
No comments:
Post a Comment