Mmea wa rangi ya kijani kibichi unaojulikana kama Gugumaji
umeelezewa kuwa kero kubwa katika ziwa Victoria.Mmea huo umeathiri kwa kiasi kikubwa shughuli za uvuvi huku
juhudi za kuuangamiza zikionekana kutofua dafu.Hata hivyo Kijana mmoja kutoka mjini Kisumu magharibi mwa
Kenya amekuwa akitumia mumea huo kutengeza bidhaa mbalimbali kama vile vikapu,
kadi na vitabu pamoja na vitu vingine.
Mwandishi wetu wa Nairobi Paul Nabiswa aliandamana kijana
huyo mike Otieno katika safari yake ya kujitafutia riziki ndani ya ziwa
Victoria .
Kundi la kinamama likivuna gugumajiJapokuwa mmea wa gugumaji
ulipovamia ziwa Victoria katika miaka ya tisini madhara yake yalikuwa dhahiri.Mwanzo
wavuvi walipata mazingira magumu ya kuvua samaki na samaki wenyewe vile vile
wakakosa nafasi ya kuzaana.Matokeo yake yakawa samaki kupungua na waliopatikana
waliuzwa kwa bei ghali mno kutokana na changamoto walizopata wavuvi katika
kuvua samaki.Hata hivyo Michael Otieno mwenye umri wa miaka 35 ameamua kungoa
mimea hiyo kutuitimia katika manufaa yake.Yeye hurauka asubuhi na mapema kutoka
kwake Migosi mtaa ambao uko kilomita mbili hivi kutoka katikati ya mji wa
Kisumu na kuelekea ziwa Victoria.
Huko ziwani huingia katika mashua na kubeba bidhaa hizo za gugumaji hapo kisha anapoondoka ziwani huzipakia kwenye gari na anapeleka nyumbani kwake.
Nyumbani kwake hakuna karakana.
Michael alinunua kifaa mfano wa tangi la maji ambako huchanganya gugumaji na karatasi zilizotumika.
Kisha husaga mchanganyiko huo na kuulowesha kwa maji.
Mabaki ya karatasi yaliyolowekwa majiHalafu kuna tangi
jingine ambako humwaga mchanganyiko aliopata katika tangi la kwanza kisha
anchunga bidhaa hiyo na matokeo yake ni karatasi anayotumia kutengeza kadi‘Sasa
hapa tunachunga kisha baadaye tunakausha huu mchanganyiko kwa jua, sasa hii
ikikauka ndiyo inakuwa karatasia ambayo tunatumia kutengenezea kadi’Michael
ambaye alikosa ajira baada ya masomo yake ya shule ya upili, anasema alipata
utalamu huu kutoka katika taasisi moja mjini Kisumu na amekuwa akifanya kazi
hii kwa miaka mitatu sasa.Kulingana naye wateja ni wachache lakini lengo lake
ni kujenga kampuni ya karatasi akiamini kuwa hiyo ndiyo njia ya kumaliza
gugumaji ziwa Victoria.
“Huu mradi utakuwa mkubwa tunajua siku moja tukiendelea hivi
tutafungua kiwanda hapa cha kutengeza makaratasi.Hapa wameleta dawa nyingi lakini
gugumaji haisikii, hata wadudu waliletwa kula huu mmea wakashindwa lakini sisi
tuking'oa itakwisha''anasema michael.
Kulingana naye mmea huo huleta ajira kwani anapopata kazi
kubwa hulazimika kuwaajiri watu wamasaidie kisha anawalipa.Wateja wake wengi ni
wakazi wa Kisumu na analenga taasisi mbalimbali za elimu.Mbali na kadi
anatengeza vitabu, vikapu na bidhaa mbalimbali.CHANZO BBC
No comments:
Post a Comment