Waandishi wawili wa Aljazeera ambao kesi yao inatarajiwa
kuanzishwa upya
Mahakama moja nchini Misri imeagiza kuachiliwa kwa dhamana
kwa wanahabari wawili wa Aljazeera kwa madai ya kulisadia vuguvugu lililopigwa
marafuku la muslim brotherhood.
Mohammed Fahmy na Baher Mohammed walifungwa jela mnamo mwezi
Juni pamoja na mwenzao raia wa Australia Peter Greste.
Lakini hatia ya kusambaza habari za uongo ili
kulisaidia
kundi la kigaidi lilitupiliwa mbali kufuatia rufaa mwezi uliopita.
Greste aliwachiliwa huru mwezi uliopita chini ya sheria
inayoruhusu kurudishwa nyumbani kwa wanahabari wa kigeni.
Bwana Fahmy ameutoa uraia wake wa Misri ili kuweza
kurudishwa nchini Canada huku Mohammed akiwa hana pasipoti ya taifa la kigeni.
No comments:
Post a Comment