Pages

Friday, February 13, 2015

Je unajua faida ya gugumaji ?

Gugumaji ilivyoisakama ziwa Victoria
 Mmea wa rangi ya kijani kibichi unaojulikana kama Gugumaji umeelezewa kuwa kero kubwa katika ziwa Victoria.Mmea huo umeathiri kwa kiasi kikubwa shughuli za uvuvi huku juhudi za kuuangamiza zikionekana kutofua dafu.Hata hivyo Kijana mmoja kutoka mjini Kisumu magharibi mwa Kenya amekuwa akitumia mumea huo kutengeza bidhaa mbalimbali kama vile vikapu, kadi na vitabu pamoja na vitu vingine.
 Mwandishi wetu wa Nairobi Paul Nabiswa aliandamana kijana huyo mike Otieno katika safari yake ya kujitafutia riziki ndani ya ziwa Victoria .


Kundi la kinamama likivuna gugumajiJapokuwa mmea wa gugumaji ulipovamia ziwa Victoria katika miaka ya tisini madhara yake yalikuwa dhahiri.Mwanzo wavuvi walipata mazingira magumu ya kuvua samaki na samaki wenyewe vile vile wakakosa nafasi ya kuzaana.Matokeo yake yakawa samaki kupungua na waliopatikana waliuzwa kwa bei ghali mno kutokana na changamoto walizopata wavuvi katika kuvua samaki.Hata hivyo Michael Otieno mwenye umri wa miaka 35 ameamua kungoa mimea hiyo kutuitimia katika manufaa yake.Yeye hurauka asubuhi na mapema kutoka kwake Migosi mtaa ambao uko kilomita mbili hivi kutoka katikati ya mji wa Kisumu na kuelekea ziwa Victoria.

Gugumaji ikikatwakatwa kabla ya kulowekwa kwenye maji yaliyochanganywa na karatasi
Huko ziwani huingia katika mashua na kubeba bidhaa hizo za gugumaji hapo kisha anapoondoka ziwani huzipakia kwenye gari na anapeleka nyumbani kwake.
Nyumbani kwake hakuna karakana.
Michael alinunua kifaa mfano wa tangi la maji ambako huchanganya gugumaji na karatasi zilizotumika.
Kisha husaga mchanganyiko huo na kuulowesha kwa maji.


Mabaki ya karatasi yaliyolowekwa majiHalafu kuna tangi jingine ambako humwaga mchanganyiko aliopata katika tangi la kwanza kisha anchunga bidhaa hiyo na matokeo yake ni karatasi anayotumia kutengeza kadi‘Sasa hapa tunachunga kisha baadaye tunakausha huu mchanganyiko kwa jua, sasa hii ikikauka ndiyo inakuwa karatasia ambayo tunatumia kutengenezea kadi’Michael ambaye alikosa ajira baada ya masomo yake ya shule ya upili, anasema alipata utalamu huu kutoka katika taasisi moja mjini Kisumu na amekuwa akifanya kazi hii kwa miaka mitatu sasa.Kulingana naye wateja ni wachache lakini lengo lake ni kujenga kampuni ya karatasi akiamini kuwa hiyo ndiyo njia ya kumaliza gugumaji ziwa Victoria.

“Huu mradi utakuwa mkubwa tunajua siku moja tukiendelea hivi tutafungua kiwanda hapa cha kutengeza makaratasi.Hapa wameleta dawa nyingi lakini gugumaji haisikii, hata wadudu waliletwa kula huu mmea wakashindwa lakini sisi tuking'oa itakwisha''anasema michael.

Kulingana naye mmea huo huleta ajira kwani anapopata kazi kubwa hulazimika kuwaajiri watu wamasaidie kisha anawalipa.Wateja wake wengi ni wakazi wa Kisumu na analenga taasisi mbalimbali za elimu.Mbali na kadi anatengeza vitabu, vikapu na bidhaa mbalimbali.CHANZO BBC

No comments:

Post a Comment