Pages

Friday, February 13, 2015

Wanahabari 2 wa Aljazeera waachiliwa

Waandishi wawili wa Aljazeera ambao kesi yao inatarajiwa kuanzishwa upya
Mahakama moja nchini Misri imeagiza kuachiliwa kwa dhamana kwa wanahabari wawili wa Aljazeera kwa madai ya kulisadia vuguvugu lililopigwa marafuku la muslim brotherhood.
Mohammed Fahmy na Baher Mohammed walifungwa jela mnamo mwezi Juni pamoja na mwenzao raia wa Australia Peter Greste.
Lakini hatia ya kusambaza habari za uongo ili 


kulisaidia kundi la kigaidi lilitupiliwa mbali kufuatia rufaa mwezi uliopita.
Greste aliwachiliwa huru mwezi uliopita chini ya sheria inayoruhusu kurudishwa nyumbani kwa wanahabari wa kigeni.

Bwana Fahmy ameutoa uraia wake wa Misri ili kuweza kurudishwa nchini Canada huku Mohammed akiwa hana pasipoti ya taifa la kigeni.

No comments:

Post a Comment