Utafiti unaonesha kwamba watu wanaopenda wanyama hasa
mbwa,utafiti unaanisha kuwa binadamu hawezi kuficha hisia zake kwa mbwa ,kwani
mnyama huyo anao uwezo mkubwa wa kushuku mambo na tofauti zetu kati ya furaha
na taswira yenye hasira.
Wanasayansi wanaofanya utafiti katika kitengo cha Messerli
Research Institute , juu ya maabara ya
mbwa wenye utambuzi ,mjini Vienna
huwafundisha mbwa kung’amua picha mbalimbali ikiwa picha aionayo ni ya mtu
mwenye furaha ama hasira .
Katika utafiti uliofanywa mfululizo,wanasayansi walionesha
mbwa taswira za watu ambazo hawakuwahi kuziona katika mafunzo yao, kumtambua
mbwa kama anaweza kugundua sura na muonekano tofauti kwenye picha hizo.
Utafiti huu,ambao ulichapishwa katika jarida la masuala ya
biolojia,ni sehemu ya utafiti mkubwa kujifunza namna rafiki wa mwanadamu ‘MBWA’
wanavyoweza kuchangamana.
Lengo kubwa la utafiti huo ni juu ya swali kubwa la
mawasiliano yao, anasema kiongozi wa utafiti huo Profesa Ludwig Huber
.Inakuwaje mbwa ajiungamanishe na mwanadamu kwa kiasi hiki? Na nini hutokea wakati
wa mchakato wa ndani?
Wanasayansi wamerudia mara ishirini kuwaonesha mbwa nusu
picha, ama iwe mdomo wa chini ama sehemu ya juu ya jicho la mtu mwenye furaha
ama uso wenye hasira,lakini mbwa waling’amua tofauti.
No comments:
Post a Comment