Wageni hawatoruhusiwa kumiliki ardhi Afrika Kusini,
kufuatana na sheria kali zinazopendekezwa na Rais Jacob Zuma.
Siku zijazo wageni wataruhusiwa tu kukodi kwa muda mrefu
ardhi ya mashamba ya Afrika Kusini.
Mbali ya hayo, mtu yeyote anayemiliki zaidi ya hekta 12,000
atalazimishwa kuiuzia serikali ili ipate kugawiwa.
Ardhi bado ni swala linalozusha hamasa nchini humo - ambako
karne tatu za ukoloni na ubaguzi wa rangi - zimeacha ardhi nyingi mikononi mwa
wachache, hasa wazungu.
Tangu kumalizika ubaguzi wa rangi mwaka 1994, chama tawala
cha ANC, kimeshindwa kufikia lengo lake la kugawa thuluthi ya ardhi ya kilimo
kwa Waafrika, ulipofika mwaka 2014.
No comments:
Post a Comment