Mrija wa mkojo (urethral) ni njia ya kutolea mkojo nje ya
mwili kutoka kwenye kibofu na unapoziba hufanya utokaji wa mkojo kuwa wa tabu
na kusababisha maumivu makali sana.
Kitaalamu kuziba kwa mrija wa mkojo huitwa urethral
stricture na husababishwa na kovu linalotokea katika sehemu ya mrija baada ya
mtu kuumia, kufanyiwa upasuaji au kupona magonjwa ya zinaa.
Magonjwa ya zinaa yanayoweza kusababisha kovu kwenye njia ya
mkojo yapo mengi na tutayajadili katika matoleo yetu yajayo kwani yapo mengi.
Hivyo ni muhimu sana mtu kutibiwa mapema anapokuwa na
magonjwa hayo. Kuziba kwa mrija huo kunaweza pia kusababishwa na uvimbe karibu
na eneo la kinena unaokandamiza mrija.
Wengi wanaopatwa na tatizo hili ni wale ambao wana historia
ya kuugua magonjwa ya zinaa au kuwahi kuwekewa mipira ya mkojo au vifaa vya
namna hiyo (catheter au cystoscope) sehemu hizo au husababishwa na kuvimba tezi
dume (BPH) kwa wanaume.
Wengine wanaopatwa na tatizo hili ni wale wanaokuwa na
historia ya kuumia au kupata majeraha maeneo ya sehemu za siri au wanaopata
maambukizi ya mara kwa mara ya magonjwa kwenye mrija wa mkojo (urethritis).
Tatizo hili mara nyingi huwakumba wanaume na ni mara chache sana kuwakumba
wanawake au watoto wachanga labda wale wanaozaliwa wakiwa na tatizo hili ambapo
kitaalamu huitwa congenital urethral
No comments:
Post a Comment