Na Haruni Sanchawa/Uwazi
MAITI ya Mchungaji James Regnald Mhando aliyefariki
Februari 18, mwaka huu imezua tafrani nzito kwa ndugu na jamaa baada ya
kujulikana kuwa alikuwa na wake wawili ambapo mke mmoja alitaka mwili uagwe
hospitali na upande wa pili ukitaka ukaagwe kwa mama yake marehemu.
Mchungaji James Regnald Mhando enzi za uhai wake.
Katika msiba huo ilibainika kuwa, mchungaji huyo (kanisa
lake tunalihifadhi kwa sababu maalum), alikuwa na watoto sita kwa mama tofauti
na wote walijitokeza katika mazishi ya baba yao.
Inadaiwa kuwa
Mchungaji Mhando alianza kuumwa Jumamosi ya Februari 14, mwaka huu lakini
inadaiwa baadhi ya watoto na ndugu wengine hawakujulishwa hadi Jumanne ambapo
inadaiwa alibebwa na gari la wagonjwa kutokea Morogoro hadi Hospitali ya Taifa
ya Muhimbili.
Jeneza la mchungaji James Regnald Mhando.
Habari zinasema ilipofika Jumatano saa tano usiku, mchungaji
huyo aliaga dunia na mbali ya kuaga dunia, bado tukio hilo lilikuwa ni siri na
ilidaiwa ilikuwa afanyiwe shughuli za mazishi kwa siri bila ya baadhi ya watoto
wake wakubwa kujua.
Hata hivyo, habari za msiba huo zilizagaa haraka na kumfikia
mke wa kwanza wa ndoa ambaye alikuwa nchini kwa ajili ya mapumziko kwani
anafanya kazi nje ya nchi, hivyo ukoo ukaanza kutaarifiana.
Mchungaji Mhando alioa na kufunga ndoa Novemba 17, 1979
katika Kanisa la Anglikana la Mtakatifu Albano, jijini Dar es
Salaam, hata hivyo, ilidaiwa kuwa mwaka 1985 mtumishi huyo wa
Mungu aliamua kuondoka nyumbani alikokuwa akiishi na mkewe na kwenda kuishi na
mwanamke mwingine ambaye inadaiwa kuwa alikuwa ni wa dhehebu lingine na
wakafunga ndoa serikalini.
Habari zinadai kwamba mwanamke huyo alikuwa anaitwa
Mwanaheri kabla ya kubadili dini na kuitwa Glory na wakafanikiwa kuzaa watoto wawili, mmoja akapewa jina la Reginald
Junior na mtoto mwingine anaitwa Sada au Doreen Mhando. Habari zinasema kabla
ya kuondoka kwa mke wa kwanza, mchungaji huyo alizaa naye watoto wawili, wa kiume
na wa kike.
..Askari akiwa eneo la tukio.
Hata hivyo, wakati wa msiba huo watoto wengine wawili
walijitokeza nao wakidai kuwa ni baba yao, hali iliyozusha minong’ono kwa watu
walioshangazwa na mwenendo wa marehemu.Akizungumza na Uwazi, mama mzazi wa
mchungaji huyo aliyejitambulisha kwa jina la Dorofea Mhando (82) alisema
kitendo kilichofanywa na mwanamke huyo ni kibaya kwani alimshawishi mwanaye
kuisaliti familia yake.
Mwanamke huyo mwingine alikuwa akiishi na mwanangu kwa siri
kubwa sana, kama vile marehemu hakuwa na
familia na akawa anajifanya kuwa yeye ndiye mke wa kwanza, kitu ambacho ni cha
uongo kwani marehemu alishaoa kanisani mwaka 1979.
“Marehemu baada ya kumpata mwanamke huyo alikuwa hashiriki
shughuli nyingi za hapa nyumbani kwa kuhofia watu watajua kuwa alikuwa na familia
nyingine, kitu ambacho kilinisikitisha,”
alidai mama huyo.
Mwili wa marehemu ukiagwa.
Mama huyo
aliongeza kuwa maisha ya mchungaji huyo yalikuwa sehemu
mbili, Morogoro na jijini Dar es Salaam,
alikuwa akifikia Mivinjeni kwenye ofisi ya shughuli zake.“Baada ya kupata
taarifa ya msiba niliagiza mwili uletwe hapa Ukonga Majumba Sita ukitokea
Muhimbili kwa ajili ya shughuli za kuagwa lakini mke mdogo akawa anapinga,”
alidai mama huyo.
Hata hivyo, ilidaiwa kuwa mke mdogo alisisitiza kuwa baada
ya kuandaa mwili wa marehemu uagwe Muhimbili, kisha upelekwe katika Makabauri ya Kinondoni kwa
mazishi. Kulitokea mabishano ambapo
mtoto mkubwa wa marehemu aliyefahamika kwa
jina Feda, alisema baba yao
hawezi kuagwa kama mkimbizi kwani ana
watoto, mke na mama yake mzazi, hivyo akaamuru mwili ukaagwe kwa bibi yake
Ukonga Majumba Sita.
Habari zinadai kuwa mvutano huo ulifikishwa Polisi Kituo
Kikuu ambapo lilifunguliwa jalada namba CD/ RB/ 2627/ 2015 ambao waliamuru
shughuli za mazishi zisifanyike hadi muafaka upatikane.
Habari zinadai kikao kilifanyika polisi na muafaka
ukapatikana kwamba mwili ukaagwe kwa mama yake mzazi Ukonga Majumba Sita.
Maofisa wa polisi walitoa askari wenye silaha chini ya
kamanda wao aliyefahamika kwa jina moja la Manyama aliyeongozana na wana
familia hao hadi Muhimbili kisha Ukonga, baadaye kwenye Makaburi ya Kinondoni
ambapo mchungaji huyo alizikwa chini ya ulinzi.
No comments:
Post a Comment