Dar es Salaam. Jumuia na Taasisi za Kiislamu Tanzania zimesema
kuwa zitahamasisha Wanajumuia wake kususia kupiga kura za maoni ya
Katiba mpya hadi pale watakapopata uhakika wa kupata Mahakama ya Kadhi
yenye meno.
Kauli ya Jumuia na Taasisi za Kiislamu zipatazo 11
imetolewa leo Jijini Dar es Salaam, na kusomwa na Naibu Katibu wa
Jumuia ya Shura ya Maimamu Wilaya ya Kinondoni, kwa madai kuwa
kinachoendelea katika mchakato wa kupatikana Mahakama hiyo ni hadaa za Serikali zinazofanyika miaka yote hasa kinapofika kipindi cha kupiga kura kwa lengo la kupata kura za waumini hao.
kinachoendelea katika mchakato wa kupatikana Mahakama hiyo ni hadaa za Serikali zinazofanyika miaka yote hasa kinapofika kipindi cha kupiga kura kwa lengo la kupata kura za waumini hao.
Akizungumza kwa niaba ya baadhi ya Jumuia 11 za
Kiislamu zilizosajiliwa na kutambulika Kisheria ambazo ni Baraza Kuu,
Tampro, Basuta, Jasuta, IPC, Haiyat Ulamaa na Shura ya Maimamu Tanzania,
Shekhe Katiba alisema kuwa watawahamasisha Waislamu wanaounda Jumuia
hizo kutopiga kura ya maoni wala kushiriki kwa namna yoyote ile katika
mchakato wa kupatikana Katiba mpya kwa sababu haiitambui Mahakama yao
yenye haki ya kuamua pindi kunapokuwa na tatizo upande wao.
Alisema kuna baadhi ya Taasisi za kidini,
magazeti, kwenye mchakato wa kutoa maoni juu ya Muswada unaohusu
Mahakama ya Kadhi, umepotoshwa kwa kuituhumu Mahakama hiyo kuwa italeta
vurugu ikiwamo kuhukumu kwa kukata watu mikono, kuhukumu wasiokuwa
Waislamu na kuwabagua wasiokuwa Waislamu , Taasisi hizo 11 ni Wahabi
hivyo maoni yao hayawakilishi waislamu wengi, kuwa umepotoshwa makusudi
ukiwa na lengo la hadaa kwa Waislamu.
“Wamefanya hivyo makusudi ili wananchi na Serikali
wasitilie maanani maoni yaliyotolewa na Taasisi hizo 11, ambayo kama
yatafanyiwa kazi na Serikali yatawezesha kupatikana kwa Mahakama ya
Kadhi inakidhi matakwa ya Sheria za Kiislamu na wajibu wake kama mamlaka
ya kutoa na kutenda haki, ”alisema Shekhe Katimba.
Nae Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Jumuia hizo
Mzee Mwinyikai, alisema kuwa katika Muswada unaoendelea kujadiliwa kwa
madai ya kupatikana Mahakama ya Kadhi Mufti amepewa jukumu la kuteua
makadhi na kutengeneza kanuni za Uendeshaji wa Mahakama ya Kadhi ili
hali Mufti sio chombo cha kisheria.
Alisema hakuna sheria inayounda ofisi ya Mufti
isipokuwa uwepo wake unategemea katiba ya BAKWATA, hivyo Mahakama ya
Kadhi uwepo wake utategemea uwepo wa Katiba ya Bakwata inayounda ofisi
ya Mufti. Kukiwa na mgogoro wa kikatiba Bakwata athari yake itaikumba na
Mahakama ya Kadhi. Hakuna duniani mtu ambaye ofisi yake haiundwi na
sheria kisha sheria ikampa mtu huyo madaraka ya kuunda chombo chenye
mamlaka ya kisheria kama Mahakama.
“Serikali inalijua hili lakini imefanya makusudi
kwa kusukumwa na nia yake ya kutopenda kuona Waislamu wanakuwa na
Mahakama ya Kadhi ya ukweli na yenye meno inayoweza kuamua kwa haki
migogoro na matatizo yake, madai ya kwamba Bakwata ni baba na Taasisi
nyingine ni watoto hayana ukweli na ndiyo maana hata Kamati ya Bunge
haikutoa mwaliko kwa Bakwata pekee , ”alisema Mwinyikai.
Katika taarifa ya Jumuia hizo iliyosainiwa na
Shekhe Abdallah Bawazir ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa Hay Atul-Ulamaa,
ilisema kuwa muswada unaojadiliwa ili kupatikana Mahakama ya Kadhi ni
kiini macho kwa sababu una baadhi ya mambo yatakayoleta mgogoro kati ya
waislamu na waislamu ikiwamo kutoa hiyari kwa mtu kufungua shauri katika
Mahakama ya Kadhi au ya Serikali
jambo hili limekusudiwa kuifanya Mahakama ya Kadhi
iwe butu na kutoa mwanya wa kutokea mgongano baina ya Mahakama ya Kadhi
na mahakama za kawaida ikiwa kila upande katika mgogoro utaamua
kufungua shauri katika mahakama tofauti.
Alifafanua Muswada huo unaitaka Mahakama ya Kadhi
ijiendeshe yenyewe bila kupata fedha kutoka Serikalini kitu ambacho
hakiwezekani ,jambo ambalo halijawahi kutokea sehemu yeyote duniani
chombo kama mahakama kujiendesha chenyewe.
“Zipo mahakama za makundi ya watu maalumu ambazo
zinaendeshwa kwa pesa za serikali ambazo ni kodi za Watanzania wote.
Mfano ni kama vile Mahakama ya Kazi, Ardhi, Biashara kwa nini mahakama
itakayotafsiri sheria za Kiislamu iwe nongwa?, ”ilisema na kuhoji
taarifa hiyo.
No comments:
Post a Comment