Taarifa zilizopatikana kwenye
sanduku linalorekodi taarifa za ndege (Black box) la ndege ya shirika
la TransAsia iliyoanguka mtoni Jijini Taipei nchini Taiwan
zimebainisha injini zake zilikatika umeme.
Wachunguzi wa taarifa za kwenye
sanduku hilo muhimu katika ndege wameeleza kuwa injini za ndege hiyo
zilishindwa kufanyakazi dakika chache tu baada ya kupaa angani.
Taarifa za katika saduku hilo
zinaonyesha marubani walivyo jaribu kuzima na kuwasha upya injini za
ndege hiyo bila ya mafanikio.
Ndege hiyo namba GE235 ilianguka
ikiwa na abiria 58 pamoja na watumishi na kuua watu 35, baada ya
kuanguka mtoni.
No comments:
Post a Comment