Pages

Saturday, February 7, 2015

NDEGE YA TRANSASIA ILIYOANGUKA INJINI ZAKE ZILIKATIKA UMEME



Taarifa zilizopatikana kwenye sanduku linalorekodi taarifa za ndege (Black box) la ndege ya shirika la TransAsia iliyoanguka mtoni Jijini Taipei nchini Taiwan zimebainisha injini zake zilikatika umeme.

Wachunguzi wa taarifa za kwenye sanduku hilo muhimu katika ndege wameeleza kuwa injini za ndege hiyo zilishindwa kufanyakazi dakika chache tu baada ya kupaa angani.

Taarifa za katika saduku hilo zinaonyesha marubani walivyo jaribu kuzima na kuwasha upya injini za ndege hiyo bila ya mafanikio.

Ndege hiyo namba GE235 ilianguka ikiwa na abiria 58 pamoja na watumishi na kuua watu 35, baada ya kuanguka mtoni.

No comments:

Post a Comment