...Wakipeana mikono baada ya kumaliza bifu lao la muda mrefu.
Choki akiteta jambo na Manyota (kulia) na Saleh kabla ya upatanisho.
BIFU lililodumu kwa muda mrefu kati ya Mkurugenzi wa Bendi ya Twanga Pepeta, Asha Baraka na Mkurugenzi wa Bendi ya Extra Bongo, Ali Choki leo limemalizika rasmi katika ofisi za Global Publishers Ltd zilizopo Mwenge, Bamaga jijini Dar.
Juhudi za kuwapatanisha wakongwe hao katika muziki wa dansi zimefanywa na baadhi ya viongozi wa Global Publishers ambap wanakiri kuwa halikuwa jambo rahisi kuwapatanisha viongozi hao.
Wakongwe hao katika muziki wa dansi wameamua kumaliza tofauti zao na kuwa kitu kimoja huku wakiahidi kushirikiana katika muziki na mambo mengine.
Mbali na mengi yaliyoongea pia wamekubaliana kufanya onyesho la pamoja huko mbeleni kuwadhihirishia mashabiki kuwa kwa sasa hawana bifu lolote na wamekuwa kama ilivyokuwa awali.
Mtandao huu unawapongeza na kuwatakia kila la kheri viongozi hao kwa uamuzi sahii waliouchukua ili kuzidi kusukuma gurudumu la muziki wa dansi.
(PICHA NA GPL)
No comments:
Post a Comment