Kijana huyu
mwenye umri wa miaka 15 anafahamika kama shabiki wa Arsenal kwa muda mrefu na
alisaini kuichezea timu hiyo mwaka jana
akianzia kwenye kikosi cha wachezaji
wenye umri chini ya miaka 16.
Hivi
karibuni Brooklyn alipakia picha kwenye mtandao wa Instagram akiwa na wachezaji
wenzie akiwa kwenye vyumba vya kubadilishia nguo vya uwanja wa mazoezi wa
Arsenal.
Akiwa amekaa
kwenye chumba hicho na wachezaji wenzie Beckham alionekana akiwa mwenye furaha
kuwa na wachezaji wenzie na dalili zote zinaonyesha kuwa huenda atafuata nyayo
za baba yake ambaye ni moja kati ya wachezaji waliopata mafanikio makubwa
kwenye mchezo wa soka.
Brooklyn Beckham akiwa na wachezaji wenzie wa kikosi cha
wachezaji wenye umri chini ya miaka 16 wa Arsenal.
Brooklyn huko nyuma amewahi kufanya majaribio na timu za
Chelsea, Manchester United, Fulham na Queens Park Rangers na alifanya majaribio
na Arsenal ambao wamemsainisha mkataba tangu mwezi mwezi novemba mwaka jana.
Cha kushangaza kuhusu familia ya Beckham ni kwamba watto
wake wote wa kiume ni mashabiki wa Arsenal na hakuna yoyote aliyechagua kufuata
nyayo za baba yao ambaye ni shabiki na gwiji wa Manchester United.
Beckham akiwa na Brooklyn wakitoka kuangalia mechi uwanjani
huko England.
Sio kushabikia tu bali watoto hawa wamekwenda mpaka hatua ya
kujiunga na timu hiyo ambapo Cruz mwenye umri wa miaka 9 anachezea kikosi cha
vijana wa Arsenal chini ya miaka 10 na Romeo mwenye umri wa miaka 12 anachezea
kikosi cha The Gunners kwa watoto chini ya miaka 13 na kaka yao Brooklyn
anachezea kikosi cha vijana chini ya miaka 16.
No comments:
Post a Comment