Baadhi ya wanajeshi wa JKT wakiingia hospitalini.
VIJANA mbalimbali ambao walipata mafunzo kutoka Jeshi la
Kujenga Taifa (JKT), leo wamekutana katika eneo la Msimbazi Center jijini Dar
es Salaam, kisha kuelekea katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa ajili ya
kumjulia hali mwenyekiti wao George Mgoba ambaye alitekwa na watu
wasiojulikana.
GPL ilifanikiwa kufika eneo la Msimbazi Center
walipokusanyika askari hao na baadaye kuelekea Hospitali ya Muhimbili. Hata
hivyo, wanahabari walishindwa kuzungumza na mwenyekiti huyo kwa sababu za
kiusalama.
(Habari/Picha: waandishi wetu/GPL)
No comments:
Post a Comment