Dar es Salaam. Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Profesa
Benno Ndulu amesema hivi sasa sekta ya Utalii ndiyo inayoongoza kwa
kuliingizia taifa mapato ya kigeni baada ya kuipita sekta ya dhahabu
iliyoshuka kutokana na kuporomoka kwa bei kwenye soko la dunia.
Akizungumza leo kwenye mkutano uliojadili
mabadiliko ya kiuchumi Tanzania, Profesa Ndulu amesema sekta ya utalii
inaliingizia taifa dola
2bilioni,
dhahabu (dola 1.7bilioni), bidhaa za viwandani (dola 1.3bilioni) na huduma za usafirishaji mizigo ni dola 800milioni.
2bilioni,
dhahabu (dola 1.7bilioni), bidhaa za viwandani (dola 1.3bilioni) na huduma za usafirishaji mizigo ni dola 800milioni.
Sekta ya utalii inaingiza Dola za Marekani 2
bilioni kwa mwaka ikifuatiwa na dhahabu inayoipatia nchi Dola za
Marekani 1.7 bilioni, bidhaa za viwanda vinazouzwa katika nchi
mbalimbali barani Afrika inaingiza Dola za Marekani 1.3bilioni
ikifuatiwa na usafirishaji wa huduma za mizigo katika nchi jirani ambapo
zinaingiza Dola za Marekani 800milioni.
Profesa Ndulu amesema ongezeko la mapato kwenye
viwanda ni sawa na fedha zote za kigeni zinazotokana na mazao sita
makubwa ya kilimo nchini kwa pamoja.
“Mfumo wa kuingiza mapato ya fedha za kigeni
nchini umebadilika sana, mimi na imani kuwa nafasi yetu kijiografia
inatupa fursa kubwa sana ya kuhudumia wengine walioko mbali na bahari,”
alisema Profesa Ndulu.
Akizungumzia kuhusu nafasi ya kilimo, Profesa
Ndulu almeema iwapo viwanda vingi vitajengwa karibu na wakulima, mfumo
wa uchumi katika maeneo hayo utaimarika kuliko ilivyo sasa.
Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa
Ibrahimu Lipumba, alisema jambo muhimu linalotakiwa kujadiliwa ni namna
gani pato la viwanda litaongezwa zaidi kwa kuwa hivi sasa kuna
changamoto ya ukosefu wa umeme wa kutosha.
“Kwa muda mrefu umeme umekuwa mdogo na ufisadi
umeathiri sana sekta ya umeme kiasi kwamba Tanesco inashindwa kuzalisha
umeme wa kutosha kwa bei nafuu,” amesema Profesa Lipumba.
Pia, amesema uwepo wa bandari inayotumiwa na nchi
jirani haujafanikiwa kuliingizia taifa mapato ya kutosha kutokana na
udhaifu ya kiuongozi.
“Uongozi wa bandari unabadilika kila wakati, kila
waziri akija anatafuta mtu wake ambaye atamsaidia katika ulaji kwa hiyo
anabadilisha uongozi uliopo analeta wengine matokeo yake bandari yetu
haiongozwi kwa ufanisi unaohitajika,” amesema Profesa Lipumba.
Mwenyekiti wa Kamati ya Hesabu za Serikali (PAC),
Zitto Kabwe, amesema matokeo yaliyotolewa na BoT yanaonyesha kuwa uchumi
hivi sasa unakwenda kwa watu wachache na kuondoka kwa watu wengi ambao
ndio wapo kwenye sekta ya kilimo, hivyo si jambo la kulifurahia.
“Taarifa hii inaashiria kwamba watakao nufaika na
uchumi ni watu wachache, wamiliki wa migodi, kampuni za kigeni
zinazohusika na utalii na wafanyabiashara wachache hasa kwenye sekta ya
usafirishaji na hivi sasa asilimia 99 ya mizigo yote inasafirishwa kwa
malori,” amesema Zitto
No comments:
Post a Comment