Pages

Tuesday, February 3, 2015

RAIS WA UJERUMANI JOACHIM GAUCK AWASILI NCHINI USIKU WA JANA


Rais wa Ujerumani Mh. Joachim Gauck akiwa ameambatana na mkewe Bibi Schadt wakiwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere usiku huu jijini Dar es salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal (kulia) akiwa mwenye furaha mara baada ya kumpokea Rais wa Ujerumani Mh. Joachim Gauck na Mkewe Bibi Schadt (walioshika maua), uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere.


Rais wa Ujerumani Mh. Joachim Gauck akiwa na mkewe Bibi Schadt na Makamu wa Rais wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal wakitazama vikundi mbalimbali vya burudani wakati wa mapokezi ya Rais huyo wa Ujerumani uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere usiku huu jijini Dar es salaam.
Rais wa Ujerumani Mh. Joachim Gauck na Makamu wa Rais wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal wakifurahia jambo walipokuwa wakitazama vikundi mbalimbali vya burudani vilivyokuwa vikitumbuiza wakati wa mapokezi ya Rais huyo uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere usiku huu jijini Dar es salaam.
Baadhi ya wakazi wa jiji la Dar es salaam waliojitokeza kumpokea Rais wa Ujerumani Mh. Joachim Gauck wakiwa na nyuso za furaha. Picha na Aron Msigwa - MAELEZO.

No comments:

Post a Comment