Jeshi nchini Uganda linasema kuwa limegundua mabaki ya
kamanda wa cheo cha juu wa kundi la waasi wa Lords Resistance Army LRA.
Okot Odhiambo ambaye alikuwa mmoja wa makamanda watano
waliokuwa wakitafutwa na mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita ICC huenda
aliuawa kwenye mapigano mwaka 2013.
Uchunguzi wa DNA unafanywa kuthibitisha mabaki hayo.
Kiongozi wa LRA Jospeh Kony
Kamanda mwingine wa LRA Dominic Ongwen
alifikiswa mbele ya
mahakama ya ICC wiki iliyopita.
Hata hivyo kiongozi wa LRA Joseph Kony bado yuko mafichoni.
No comments:
Post a Comment