Runinga
Mamlaka ya mawasiliano nchini Kenya sasa inasema kuwa
itavipiga faini vituo vya uninga vya NTV,KTN,Citizen na QTV nchini Kenya kwa
kuzima matangazo yao kufuatia hatua ya serikali kuhamia katika matangazo ya
dijitali.
Mkurugenzi wa mamlaka hiyo Francis Wangusi amewaambia wana
habari kwamba hatua zitachukuliwa dhidi ya runinga hizo kwa kukiuka sheria.
''Lazima waadhibiwe'',alisema Wangusi baada ya runinga hizo
kufunga matangazo na hivyobasi kuwanyima wakenya fursa ya kuona taarifa zao
katika vituo vya DSTV,Zuku na vituo vyengine vya kurusha matangazo.
Mda mfupi baada ya vituo hivyo kuzimwa siku ya jumamosi,DSTV
iliweka taarifa katika mtandao wa twitter ikiwataka wakenya wanaohitaji
kuangailia habari kujaribu kufanya hivyo kupitia vituo vyengine vya runinga.
Vituo vivyo viliendelea kufunga matangazo yao siku ya
jumapili baada ya maafisa wa mamlaka hiyo ya mawasiliano kufunga mitambo yao ya
kurusha matangazo hewani katika eneo la Limuru.
No comments:
Post a Comment