Dar es Salaam. Wakala wa Ukaguzi wa Madini nchini (TMAA)
umetangaza dau nono kwa yeyote atakayewezesha kukamatwa kwa
mfanyabiashara yeyote anayesafirisha madini kwa njia za magendo kupitia
njia za panya zaidi ya 400 zilizopo nchini.
Hayo yalisemwa jana na Mkurugenzi wa Fedha na
Utawala wa TMAA, Bruno Mteta alipokuwa akitoa taarifa ya mwaka uliopita
ya mapambano dhidi ya magendo ya madini mbele ya waandishi wa habari.
“Kwa kipindi cha kuanzia Januari mpaka Desemba
mwaka jana, wakala umeweza kukamata watoroshaji
wa madini ya aina mbalimbali katika matukio 27 tofauti. Tunawaomba Watanzania wazalendo kushirikiana nasi ili kuwabaini watu wote wanaojishughulisha na magendo haya na tayari wizara imethibitisha zawadi ya asilimia tano ya thamani ya madini yatakayokamatwa itatolewa,” alisema Mteta.
wa madini ya aina mbalimbali katika matukio 27 tofauti. Tunawaomba Watanzania wazalendo kushirikiana nasi ili kuwabaini watu wote wanaojishughulisha na magendo haya na tayari wizara imethibitisha zawadi ya asilimia tano ya thamani ya madini yatakayokamatwa itatolewa,” alisema Mteta.
Wakala umeanza utekelezaji wa mkakati huo
ulioratibiwa tangu mwaka 2012 wakati huo Serikali ilisema itatoa
asilimia 30 ya thamani ya mzigo baada ya kugundua kuwapo kwa watu
wanaolipwa asilimia 10 kusaidia kufanikisha magendo hayo na hivyo
kuchangia kuikosesha mapato.
Alisema hilo lilikuwa ni pendekezo linaloendelea
kutekelezwa na kwamba, kiasi hicho ni haki ya mtoa taarifa ambaye
hatotajwa mahali popote katika mchakato mzima wa hatua za kisheria.
“Utoroshaji wa madini umekithiri, zinahitajika
nguvu za pamoja ili kuhakikisha Taifa linanufaika na rasilimali zake.
Atakayekamatwa mali yake itataifishwa na kama ni kampuni basi
itanyang’anywa leseni yake na kutoruhusiwa tena kufanya shughuli zake
hapa nchini,” alisema Mteta.
Kwa madini yanayoingizwa ili yasafirishwe nje bila
kuwa na vibali, alisema nayo yakikamatwa yatataifishwa hivyo kuwataka
wote wanaofanya hivyo kutumia ofisi za ukaguzi zilizoko mipakani
kuhalalisha madini waliyonayo.
Meneja wa Uthaminishaji, George Kaseza alisema
njia za panya ni nyingi na wakala huo peke yake hauwezi kufanikiwa
kudhibiti, hivyo aliwataka wananchi kushiriki kuziba njia hizo kwa kutoa
taarifa kwa Jeshi la Polisi au ofisi ya wakala iliyo karibu.
“Nwaka jana tulikamata madini yenye thamani ya zaidi ya Sh850 milioni katika viwanja vyetu vya ndege pekee,” alisema.
Alisema wakala umejitahidi kuimarisha ulinzi na
ukaguzi katika viwanja vya ndege kwa kushirikiana na taasisi nyingine za
Serikali kama Jeshi la Polisi, Mamlaka ya Viwanja vya Ndege (TAA),
Idara ya Usalama wa Taifa, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na Idara ya
Uhamiaji.
“Juhudi hizo zimewezesha kukamatwa kwa madini yenye thamani ya Sh8.4 milioni.
“Hiyo ilikuwa ni baada ya kupata taarifa kutoka
kwa mwananchi aliyetilia shaka mienendo ya mtuhumiwa. Kesi ipo
mahakamani mpaka sasa,” alisema.
No comments:
Post a Comment