Na Bertha Lumala, Dar es Salaam
Muda
mfupi baada ya uongozi wa Yanga SC kudai kuhujumiwa na Bodi ya Ligi Kuu
Tanzania (TPLB), bodi hiyo imewajibu wanajangwa kwamba "mkuki kwa
nguruwe, kwa binadamu mchungu."
Mapema
leo, uongozi wa Yanga SC umetishia kutoingiza timu uwanjani katika mechi
yao ya Ligi
Kuu Tanzania Bara dhidi ya JKT Ruvu Stars iliyopangwa kuchezwa Uwanja wa Taifa Machi 11, kutokana na kile ulichodai kutoshirikishwa katika uamuzi wa mabadiliko ya ratiba.
Kuu Tanzania Bara dhidi ya JKT Ruvu Stars iliyopangwa kuchezwa Uwanja wa Taifa Machi 11, kutokana na kile ulichodai kutoshirikishwa katika uamuzi wa mabadiliko ya ratiba.
Jery
Muro, Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Yanga SC, amesema jijini
hapa leo kuwa uongozi wa Yanga SC ulikuwa unatambua kwamba kikosi chake
kingecheza dhidi ya JKT Ruvu kesho kabla ya kuivaa Simba SC Jumapili,
lakini kimeshangaa baada ya kusoma kwenye mitandao kwamba mechi yao
dhidi ya JKT Ruvu Stars haipo KESHO.
Hat hivyo, Fatma Shibo, Kaimu Ofisa Mtendaji wa TPLB, amesema mabadiliko ya ratiba ya Ligi Kuu Tanzania Bara hayajafanywa kwa siri na yametokea kutokana na ushiriki wa timu nne za ligi hiyo, Azam FC, Mtibwa Sugar FC, Simba SC na Yanga SC katika michuano ya Kombe la Mapinduzi mapema mwaka huu.
Hat hivyo, Fatma Shibo, Kaimu Ofisa Mtendaji wa TPLB, amesema mabadiliko ya ratiba ya Ligi Kuu Tanzania Bara hayajafanywa kwa siri na yametokea kutokana na ushiriki wa timu nne za ligi hiyo, Azam FC, Mtibwa Sugar FC, Simba SC na Yanga SC katika michuano ya Kombe la Mapinduzi mapema mwaka huu.
Fatma
amekanusha madai ya Yanga SC kwamba mechi yao dhidi ya JKT Ruvu Stars
wanayodai ilipangwa kuchezwa kesho kwamba yamefanywa kwa siri, kwa vile
uongozi wa wanajangwani ulitaarifiwa tangu Febuari 16 juu ya mabadiliko
ya ratiba ya ligi.
"Mabadiliko
ya ratiba ya ligi kuu yametokea kutokana na ushiriki wa timu nne za
Tanzania Bara katika michuano ya Kombe la Mapinduzi visiwani Zanzibar
Januari mwaka huu," Fatma amesema.
"Hili la
pili la Yanga kudai hatukuwashirikisha katika kupangua mechi yao dhidi
ya JKT Ruvu si kweli kwa sababu tuliwasiliana na uongozi wa Yanga tangu
Februari 16. Labda wawe na tatizo la kutofungua email, lakini Katibu
Mkuu wao (Jonas Tiboroha) alisema aliona email yetu kuhusu suala hilo,"
amesema zaidi Fatma.
Ofisa
huyo amesema bodi haina njama zozote za kuihujumu Yanga SC katika mechi
zake kwani waliibeba pia katika kuilazimisha Tanzania Prisons FC irejeec
Mbeya kutoka Dar es Salaam kucheza dhidi yao mechi waliyoshinda 3-0
jijini Mbeya juzi.
"Kama ni
watu wa kulalamika, walipaswa kulalamika Prisons kwa sababu walikuwa
hapa Dar es Salaam, lakini tukawaambia warejee kwao Mbeya kucheza dhidi
ya Yanga baada ya uongozi wa Yanga kutuomba wacheze mechi zao zote zsa
Mbeya kabla ya kwenda Botswana.
"Mpaka
sasa bodi inadaiwa pesa ya gharama za usaffiri na timu ya Prisons kwa
sababu tuliwafanya wasafiri mara mbili kutoka Dar es Salaam kwenda Mbeya
na kurudi tena hapa Dar es Salaam," amesema zaidi Fatma.
Katika
hoja zake, Muro amedai TPLB ni janga la kitaifa na kwamba kusogezwa
mbele kwa mechi hiyo dhidi ya kikosi cha Felix Minziro cha JKT Ruvu, ni
hujuma dhidi ya Yanga SC, kwa kuwa timu hiyo ya Jangwani jijini hapa
itakuwa na siku mbili tu za kupumzika baada ya kucheza dhidi ya maafande
hao kabla ya kuivaa Platinum ya Zimbabwe katika mechi yao ya kwanza ya
raundi ya kwanza ya michuano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika
Jumamosi.
Huku
akihoji kiwango cha elimu cha Kaimu Ofisa Mtendaji wa TPLB, Fatma na
watendaji wengine wa bodi hiyo, Muro amesema tayari uongozi wa Yanga SC
umewasilisha barua TFF tangu jana kusaka ufafanuzi wa mabadiliko ya
ratiba hiyo.
"Kwa sasa
mpinzani wetu ni Azam FC na siyo Simba, mechi dhidi ya Simba kwetu ni
kwa sasa kama bonanza, siyo kipaumbele chetu, sisi tunawasubiri siku
hiyo ifike tucheze nao, lakini hawana jipya kwa tunawazidi pointi
nyingi,"ametamba Muro.
"Azam
kesho na keshokutwa tunamwacha mbali maana mpaka sasa tuko mbele yake
kwa pointi nne katika msimamo wa ligi, sisi wapinzani wetu na klabu
ambazo unaweza kuzilinganisha na sisi ni Kaizer Chief ya Afrika Kusini
au TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ambazo zinacheza
michuano ya kimataifa," amesema zaidi Muro.
Chanzo:Shaffihdauda.com
No comments:
Post a Comment