Sunderland imemfukuza kazi meneja wake Gus Poyet baada ya
kushinda mechi moja tu kati ya 12 za Ligi Kuu ya England. Paka Weusi hao
wananinginia katika nafasi ya 17 baada ya kufungwa 4-0 na Aston Villa siku ya
Jumamosi. Poyet amekutana na mkurugenzi
mkuu Margaret Brrne pamoja na wajumbe
wengine wa bodi baada ya mazoezi siku ya Jumatatu, lakini klabu hiyo iliamua
kumsimamisha kazi. Poyet, raia wa Uruguay alichukua umeneja wa Sunderland mwezi
Oktoba 2013, kuziba nafasi ya Paolo di Canio.
No comments:
Post a Comment