Akiuliza swali bungeni jana, Rwamlaza alihoji serikali inasemaje kuhusiana madai hayo.
Akijibu
swali hilo, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Pereira Ame Silima, alisema
Sheria za Usalama wa Barabarani namba 67 ya mwaka 1973 inatoa
mamlaka kwa askari wa barabarani kutoza faini za papo kwa papo kwa makosa mbalimbali ya usalama wa barabarani.
mamlaka kwa askari wa barabarani kutoza faini za papo kwa papo kwa makosa mbalimbali ya usalama wa barabarani.
“Hili ni moja ya
jukumu la msingi la kikosi cha usalama wa barabarani unaolenga
kuimarisha usimamizi wa Sheria za Usalama wa Barabarani,” alisema.
Alisema
ukamataji wa makosa ya barabarani na faini ya papo kwa papo hulenga
katika kuwatia hofu ya adhabu madereva wakorofi hivyo kuwafanya wafuate
sheria na kanuni za usalama barabarani.
“Hakuna
kiwango cha pesa ambacho askari wa usalama wa barabarani amepangiwa
kukusanya, askari ameelekezwa kukamata makosa kwa wingi iwezekanavyo
hususani makosa hatarishi kama vile mwendo wa kasi, ulevi, ujazaji wa
abiria na mizigo, uendeshaji wa hatari na kadhalika,”alisema.
Katika
swali la nyongeza, Mbunge wa Viti Maalum , (CUF), Mkiwa Kimwaga,
alisema askari wa vitochi barabarani wamekuwa ni kero kubwa kwa
madereva.
“Wakati mwingine wanasimamisha magari kama sita na wanakwambia kuwa na wewe umekuwa ukiendesha katika mwendo kasi,”alisema.
Alihoji
ni lini serikali itanunua vitochi vya kisasa ambavyo vitatoa na namba
badala ya vya sasa ambavyo vinaonyesha mwendo tu kama walivyoahidi
katika bajeti iliyopita.
Akijibu swali hilo, Silima alisema wananchi hawatakiwi kuona kero kwa vitochi kwa sababu viko pale kwa ajili ya kuepusha ajali.
“Fikra kwamba vitochi ni kero mziondoe kabisa, tunakerwa ili tusife tunataka maisha yenu yaendelee,”alisema.
Alisema
ajali nyingi zinazotokea nchini zinasababishwa na mwendo kasi. Hata
hivyo, alisema serikali imeshanunua baadhi ya kamera za kisasa
zinazoonyesha namba za gari.
Alisema kuwa kamera hizo zinaweza kurekodi namba na mwendo na kesho yake dereva akaelezwa makosa yake
No comments:
Post a Comment