Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Wednesday, March 4, 2015

MWENYEKITI WA MABASI YA UDA, ROBERT KISSENA ANATAFUTWA NA JESHI LA POLISI KWA UTAPELI WA MIL.740


*POLISI DAR YATAKA AJISALIMISHE KWA KWENDA KUJIBU TUHUMA DHIDI YAKE.

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

Mwenyekiti wa Bodi ya Usafiri Dar es Salaam (UDA), Robert Saimon Kissena (Pichani) anasakwa na Jeshi la polisi kwa utapeli wa sh.milioni 740 kwa kampuni ya kutengeneza mafuta.

Robert Kissena inadaiwa alikwenda katika kampuni ya kuzalisha mafuta ya pamba na kusema ana mbegu tani 200 ambazo alidai atauza kwa zaidi ya sh.300,000
.
Kampuni hiyo ilianza kufatilia suala hilo juu ya kupata tani hizo kupitia katika kampuni yake Saimon Agency Group Limited ambapo walikwenda mpaka maswa na kuambiwa hana kibali cha kuwa na mbegu hizo.

Akizungumza na waandishi wa habari Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Kahama Oil Meals Limited wanaojihusisha Uchambuaji na Kukamua Mafuta ya Pamba, Amos Maganga alisema Robert Kisesena amewatapeli milioni 740 kwa kusema kitu ambacho hana na badala yake kuanza danadana ya maneno.

Alisema baada ya kuona danadana za Robert Kissena kupitia kampuni yake walifungua kesi mkoani Tabora ambapo ilikwenda na kuzimwa na mtu mmoja ambaye wanadai ni kigogo wa Serikali ya Jamhuri Muungano ya Watanzania.
Kamanda Mkuu wa Kanda Maalum ya Mkoa wa Dar es Salaam Suleiman Kova akiongea na waandishi wa habari juu ya kusakwa kwa Mwenyekiti wa Mabasi ya Dar es Salaam (UDA) Robert Kissena.


Alisema tukio la kitapeli la ambaye sasa ni mwenyekiti wa bodi UDA alilifanya Julai 31 mwaka jana huko Maswa Mkoani Shinyanga kwa kudai ana mbegu za pamba ambazo zimeota mbawa hadi sasa.

Kisena alisema aliendelea kutaka kufanya utapeli wa kutaka kuuza tani moja zaidi ya sh. 400,000 na ndipo wakamtaka awarudishie fedha zao
.
Kissena anadaiwa kutambulisha watu wawili ambao ni Mkurugenzi Saimon Agency Group Limited Kulwa Saimon Kissena na katibu wa kampuni hiyo Patrick Kissa Mtani kupitia kampuni iliyofanya utapeli huo.
Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Kahama Oil Meals Limited (Kushoto) akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari jijini Dar es Salaam juu ya malalamiko yao kutapeliwa kiasi cha Milioni 740 kwa kuuziwa mbegu za pamba feki. Pembeni yake ni Meneja Mkuu wa Kampuni ya Kahama Oil Meals Limited, William Matunage.

Maganga baada ya kuona hali inazidi kuwa ngumu upatikanaji wa fedha hizo walikwenda kufungua kesi mkoani Simiyu na kutolewa kwa kibali cha kukamatwa kwa mwenyekiti wa UDA na wenzie
.
Alisema walikuja Dar es Salaam Februari 25 mwaka huu wakiwa na hati ya mahakama na kufika katika kanda ya Maalum ya Polisi ambapo zoezi la ukamataji lilifanyika na baada ya hapo Robert Kissena ambaye ni Mwenyekiti wa Bodi ya UDA alidai anajisikia vibaya kutokana na Sukari na shinikizo la damu na kuomba adhaminiwe pamoja na wenzie.
Meneja Mkuu wa Kampuni ya Kahama Oil Meals Limited, William Matunage nae alijibu maswali ya waandishi wa habari.

Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam,Suleiman Kova alisema kuwa watu walimdhamini na kutoa ushauri wa kwenda kwa ndege kwa mtuhumiwa huyo ndilo lilifanyika.

Alisema siku ya pili baada ya kudhaminiwa walikwenda wadhamini wakiwa hawanawatuhumiwa na kuwauliza wako wapi walidai Robert Kisena kalazwa Hospitali ya Ami Jijini Dar es Salaam na kuanza kupata shaka ndipo waliwafungulia mashitaka ya kutorosha mtuhimiwa.

Kova amesema Robert Kissena Mwenyekiti wa Bodi ya UDA mwenye jina la kuaminika ajisalimishe katika jeshi la polisi na kwenda kujibu mashitaka kwa mujibu wa hati ya mahakama.

No comments:

Post a Comment