Askofu wa Kanisa Katoliki jimbo la Mbinga Mhashamu John Ndimbo akiongoza ibada ya mazishi ya aliyekuwa mbunge wa Mbinga Magharibi marehemu Kapteni John Damiano Komba wakati wa ibada ya mazishi yake yaliyofanyika kijijini kwake Lituhi wilayani Nyasa Mkoani Ruvuma
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete wakiweka udongo katika kaburi la aliyekuwa mbunge wa Mbinga Magharibi marehem Kapteni John Damiano Komba wakati wa ibada ya mazishi yake yaliyofanyika kijijini kwake Lituhi wilayani Nyasa ,Mkoani Ruvuma.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete wakiweka shada la maua katika kaburi la aliyekuwa mbunge wa Mbinga Magharibi marehemu Kapteni John Damiano Komba wakati wa ibada ya mazishi yake yaliyofanyika kijijini kwake Lituhi wilayani Nyasa ,Mkoani Ruvuma. (Picha na Freddy Maro)
---
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete leo, Jumanne, Machi 3, 2015, ameungana na mamia ya waombolezaji kumzika Mbunge wa Jimbo la Nyasa na msanii mahiri wa muziki nchini, Mheshimiwa Kepteni John Damiano Komba, kwenye makaburi ya Kanisa Katoliki katika Kijiji cha Lituhi, Wilaya ya Nyasa, Mkoa wa Ruvuma.
Mara baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Songea, akitokea Dar es Salaam, kiasi cha saa tano na robo asubuhi, Rais Kikwete amekwenda moja kwa moja Lituhi, karibu kiasi cha kilomita 140 kutoka mjini Songea, kwa ajili ya mazishi ya Mheshimiwa Komba ambaye pia alikuwa Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama cha Mapinduzi (CCM).
Rais Kikwete amejiunga na waombolezaji akiwemo Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Anne Semamba Makinda kiasi cha saa tisa mchana kwa ajili ya mazishi ya mmoja wa wasanii ambao walijijengea heshima kubwa kwa nyimbo zake za uhamasishaji.
Wakati wa shughuli za mazishi ambazo kidini zimeongozwa na Askofu John Ndimbo wa Jimbo Katoliki Mbinga, waombolezaji walisomewa salamu za rambirambi ambazo zimetumwa na Rais wa Pili wa Malawi, Mheshimiwa Bakili Muluzi ambaye sasa amestaafu.
Katika salamu hizo, Mheshimiwa Muluzi amesema: “Nilimjua Komba kama rafiki na taarifa za kifo chake cha ghafla zimenistua sana.”
Mwili wa Marehemu Komba uliteremshwa kaburini saa 9:30 mchana huku ukishuhudiwa na mjane wa marehemu Salome Komba na watoto wake 11.
Rais Kikwete ameondoka Lituhi mara baada ya mazishi kurejea mjini Songea kumalizia ziara yake ya siku mbili ya kikazi mkoani Ruvuma.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiongozana na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye,Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana Ndugu Sixtus Mapunda pamoja na wananchi kutoka maeneo mbali mbali ya Tanzania kwenda kumzika marehemu Kapteni John Komba kijijini kwake Lituhi.
Mke wa Marehemu Kapteni John Komba ,Salome (kushoto) akiweka shada la maua juu ya kaburi la marehemu.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiweka shada la maua pamoja na mkewe Mama Salma Kikwete juu ya kaburi la Kapteni John Komba aliyezikwa kwenye makaburi ya kijiji cha Lituhi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Jakaya Mrisho Kikwete pamoja na mkewe Mama Salma Kikwete wakitoa heshima mara baada ya kuweka shada la maua kwenye kaburi la Kapteni John Komba.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiweka shada la maua kwenye kaburi la Kapteni John Damian Komba aliyezikwa kijijini kwake Lituhi.
Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara) Mwigulu Lameck Mchemba pamoja na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM Taifa Nape Nnauye wakiweka shada la maua juu ya kaburi la Kapteni John Komba aliyefariki jijini Dar es Salaam tarehe 28 februari na kuzikwa kijijini kwake Lituhi tarehe 3 Machi 2015.
Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Ndugu Said Mwambungu (kulia) akiweka shada la maua pamoja na mkewe kwenye kaburi la Kapteni John Komba.
Khadija Kopa akiwa katika huzuni kubwa mara baada ya kuweka shada la maua kwenye kaburi la Kapteni John Komba kijijini kwake Lituhi.
No comments:
Post a Comment