Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Monday, March 30, 2015

MWILI WA MAREHEMU ABDU BONGE KUSAFIRISHWA LEO KWA AJILI YA MAZISHI



 Muasisi wa Tip Top Connection, Abdul Bonge amefariki dunia juzi wakati akiamulia Ugomvi wa watu wake wa karibu ndipo alipoanguka vibaya kwenye sakafu na kupoteza Maisha, Mwili bado uko hosptalini kwa Uchunguzi zaidi. Mwili wamarehemu Abdu Bonge utasafirishwa leo kuelekea Morogoro Mbuyuni Kilometa takribani 100 kutokea Morogoro Mjini ambako ni Nyumbani kwa Marehemu kwa ajili ya mazishi. Kwa sasa msiba upo Magomeni Njiapanda ya Kagera maskani ya Tiptop Connection.

Abdul ni kaka yake na Babu Tale na kwa pamoja walianzisha kundi hilo.
Mastaa mbalimbali wametumia Instagram kutuma salamu zao za rambi rambi.

“Nimesikia habari za msiba wa my brother Abdu Bonge juzi usiku nimesikitika kweli.Nimefanya kazi na Abdu Bonge kwa miaka mingi sana wakati akiwa ndio anasimamia vijana wake wa tiptop kabla ya 

 
@babutale kuanza kusimamia kila kitu.
Alikuwa mtu fresh mwenye upendo sana.Mwenyezi Mungu ampumzishe kwa amani.Poleni wote mlioguswa na msiba huu,wana tiptop,pole sana @babutale, ” ameandika Dina Marious.

Naye Diamond ameandika: Dah! RIP Brother Bonge.. mbele yako nyuma yetu sisi…pole sana @babutale @dj_kman Mjomba iddi , @madeeali na familia nzima… amini mpo pamoja nasi katika kipindi hichi kigumu…
Chege

Nadhani waliwahi kuhusiwa kaka zangu dada zangu na ndugu zangu wengine lakini mimi nimekua nikiskia neno husia toka nikiwa mdogo,haijalishi ni husia kuhusu nini!!!nadhani maneno unayo ambiwa na mtu hlf baada ya muda mchache anafariki ndio unaitwa husia,leo ni siku ya nne kwa mara ya kwanza kukaa mimi na marehemu tukiwa wawili tu,na kuniambia vitu vingi sana tofaut na upeo wa uwezo wangu wa kufikiria,……nilifikiria sana na kuwapigia sim marafiki zangu wawili wakaribu sana @mhtemba na @madeeali na wote walitamani kuongea nae maskini yamungu mwenyezi mungu kamchukua kaka yetu ndugu yetu boss wetu ABDU BONGE leo,ulichoniambia juzi nadhani ni urithi na husia mkubwa sana katika maisha yangu,nitautumia na kujifunza siku zote,mungu akulaze mahala pema peponi kaka yangu………RIP ABDU BONGE poleni sana ndugu zetu na marafiki zetu wa karibu #tiptopconnection pigo lenu ndio pigo la #tmkwanaumefamily #yamotoband mungu mlaze pema abdu bonge..
.

Madee

Dah et nlisema Ata Abdul bonge siku yako aijulikani…dah Leo imejulikana..nsingekua mimi bila wewe…nlijivunia kua nawewe..nlijiamin popote pale..ww ndio baba wa mziki wangu…Asa nani atanielekeza nkikosea kuandika?nenda My Godfather…ntakuja..

Tunawapa pole Tip Top kwa msiba huo.

No comments:

Post a Comment