Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu
Waziri
Mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu amewasili nchini Marekani kupinga
dhidi uwezekano wa kufikia makubalino na Iran juu ya mpango wake wa
nyuklia.
Bwana Netanyahu anasema mkataba huo hautoshi kuizuia Iran kumiliki silaha za nyuklia.
Anatarajiwa
kulihutubia Bunge la Congress Jumanne, hotuba ambayo haikukubaliwa
kabla na utawala wa Rais Obama na kuiudhi Ikulu ya Marekani.
Hotuba
hiyo inakuja wiki mbili kabla ya uchaguzi wa
Israel, huku chama chake cha Likud kikiwa katika shinikizo katika uchaguzi wa nyumbani.
Israel, huku chama chake cha Likud kikiwa katika shinikizo katika uchaguzi wa nyumbani.
Marekani na mataifa mengine yanayotambulika kama P5+1 - wanajadiliana na Iran kuhusu mpango wake wa nyuklia.
Wanataka
mpango wa makubaliano kufikia mwishoni mwa mwezi huu ambao unaeleza
wasiwasi kuwa Iran inatafuta teknolojia ya silaha za nyuklia, jambo
ambalo linakanushwa na Iran.
Rais Obama hana mpango wa kukutana na Bwana Netanyahu
Wafuasi kadhaa wa Democrat akiwemo Makamu wa Rais Joe Biden amesema hatahudhuria hotuba hiyo.
No comments:
Post a Comment