Mazoezi ya kijeshi ya mwaka daima yamekuwa yakisababisha uhasama katika peninsula ya Korea.
Korea
Kaskazini imefyatua makombora mawili ya masafa mafupi katika bahari
wakati mazoezi ya pamoja ya kijeshi kati ya Marekani na Korea Kusini
yakiendelea.
Makombora hayo mawili yakiruka katika masafa ya
kilomita 490, yalifyatuliwa kuelekea baharini kutoka mji wa magharibi wa
Nampo, limesema jeshi la Korea Kusini.
Mazoezi, yanayohusisha maelfu ya askari daima yamekuwa yakiiudhi Korea Kaskazini.
Korea
Kusini na Marekani zinaelezea mazoezi hayo ya kijeshi kuwa yana lengo
la kujihami. Korea Kaskazini inayaita mazoezi hayo kuwa yana lengo la
uvamizi.
Korea Kaskazini imefanya majaribio ya nyuklia katika
mwaka 2006, 2009 na 2013. Mazungumzo ya mataifa sita yanayolenga
kumaliza mpango wa nyuklia wa Korea Kaskazini yamekwama tangu mapema
mwaka 2009.
No comments:
Post a Comment