NA ISSA MNALLY
PEPO la ugomvi linazidi kumuandama staa wa Bongo Fleva,
Khaleed Mohamed ‘TID’, baada ya kusakwa na jeshi la polisi kwa kosa la
kumjeruhi mtu mwishoni mwa wiki iliyopita, msanii huyo ametengeneza kicha cha
habari kwa mara nyingine akidaiwa kumpiga meneja wake aliyefahamika kwa jina la
Tall Mnyama.
Staa wa Bongo Fleva, Khaleed Mohamed ‘TID’.
Katika tukio la awali, TID alidaiwa kutembeza kichapo na
kumjeruhi James Richard, mkazi wa Jiji la Dar kwa kosa alilodai kuwa ni kupaki
gari kwenye eneo lake, maeneo ya nyumbani kwa msanii huyo, Kinondoni-Sterio
jijini Dar.
Tukio la kumpiga meneja wake, TID anadaiwa kulifanya katika
Hotel ya Element, Oysterbay ambapo inaelezwa kuwa msanii huyo alifika hotelini
hapo akiwa na wapambe wake na alipomkuta meneja huyo, alibishana naye kwa muda
mfupi kisha kumzaba kibao.
“Alimkuta mwenzake (Tall) kaka sehemu, akamsemesha na
alipojibu tu akamzaba kofi, lakini huyu meneja wake alikuwa mstaarabu,
hakumlipizia. Baada ya tukio hilo TID alitokomea na kama unavyojua sasa hivi
anaishi kama digidigi, mbaya zaidi watu wanasema asipompiga mtu hasikii raha,”
kilidai chanzo chetu.
Chanzo hicho kilizidi kumwaga ‘ubuyu’ kuwa, meneja huyo
baada ya kupokea kipigo hicho, alikwenda kutoa taarifa katika Kituo cha Polisi
Oysterbay kilicho chini ya Camillius Wambura (pichani) ambapo lilifunguliwa
jarada lililosomeka; OB/RB/3922/2015/TAARIFA.
Mwanahabari wetu alipomtafuta meneja huyo kuhusiana na tukio
hilo, alikiri kuwa limemtokea lakini akasema hakutaka kulivalia njuga lakini
alichokifanya ni kutoa taarifa polisi ili endapo atarudia, amchukulie hatua
kali zaidi za kisheria.
“Ni kweli TID alinishambulia kwa kunipiga kibao, iliniuma
sana lakini nimeamua kumsamehe, nilichokifanya ni kutoa taarifa polisi ili kama
atarudia nimfikishe katika vyombo husika,” alisema meneja huyo.
Jitihada za kumpata TID ili aweze kuzungumzia tukio hilo
hazikuzaa matunda kufuatia simu yake kutopatikana hewani.Jitihanada za kumpata
Wambura hazikufanikiwa baada ya simu yake kuita bila kupokelewa kwa siku ya
juzi.
No comments:
Post a Comment