Mwananchi akiwa amebeba moja ya barafu la mvua,yaliyokuwa
yanadondoshwa na mvua kubwa iliyonyesha usiku wa kuamkia leo katika Kata ya
Mwakata wilayani Kahama mkoani Shinyanga.
Mawe hayo ya mvua yanadaiwa kuwa na ukubwa wa ndoo ya lita
10,na yalikuwa yamezagaa katika kijiji hicho baada ya mvua kukatika.Pichani ni
barafu ikiwa imeanza kuyeyuka
Miili ya watu 7 wa familia moja waliokufa katika tukio hilo
Watu 38 wamefariki
dunia na wengine 82 wamejeruhiwa baada ya kuangukiwa na nyumba kutokana na mvua
kubwa ya mawe iliyoambatana na upepo kunyesha usiku wa kuamkia leo katika
kijiji cha Mwakata Kata ya Mwakata wilayani Kahama mkoani Shinyanga.
Mbuzi wakiwa wamekufa
Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi ya wilaya ya Kahama, ambaye
ni mkuu wa wilaya hiyo Benson Mpesya(mwenye suti) amesema kamati ya ulinzi na
usalama ya wilaya itakaa kabla ya kamati ya mkoa ili kupata taarifa
zitakazoisaidia serikali kuanza kutoa misaada. eneo la tukio
Picha zote na Faraji Mfinanga,Shabani Alley na Mohab
Dominic-Malunde1 blog Kahama
No comments:
Post a Comment