Wapiganaji
wa kiislamu wameripotiwa kuviteka visima viwili vya mafuta katikati mwa
Libya huku makundi hasimu yakiendelea kupigania udhibiti wa taifa hilo.
Vikosi vinavyolinda visima vya mafuta vya al Bahi na al Mabruk vilisalimu amri baada ya kuishiwa na silaha.
Serikali
ya Libya inayotambulika kimataifa mjini Tobruk inakabiliana na mahasimu
wake wa Libya Dawn ambao wanadhibiti mji mkuu wa Tripoli.
Pande hizo mbili pia zilishambuliana siku ya jumanne.
''Watu
wenye itikadi kali walichukuwa udhibiti wa maeneo ya al Bahi na al
Mabruk na sasa wanaelekea kudhibiti kisima cha mafuta cha Al Dahra
kufuatia kusalimu amri kwa vikosi vilivyokuwa vikilinda maeneo
hayo'',alisema kanali al_Hassi, msemaji wa usalama wa sekta ya mafuta.
No comments:
Post a Comment