Mgonjwa anayeugua ugonjwa wa kiharusi
Watu wanaolala kwa zaidi ya masaa manane kwa siku wana
uwezekano mkubwa wa kupata ugonjwa wa kiharusi,utafiti umesema lakini wataalam
hawajua sababu yake.
Utafiti uliofanywa kwa takriban watu 10,000 katika chuo
kikuu cha Cambridge ulibaini kwamba wale wanaolala kwa takriban saa nane wana
uwezekano mkubwa wa asilimia 46 kupata kiharusi.
Watu wazima hupendelea kulala kati ya saa sita na tisa ili
kupumzika vizuri,lakini kulala zaidi hushirikishwa na matatizo ya afya kama
vile ugonjwa wa sukari pamoja na ule wa kunenepa kupitia kiasi.
Hatahivyo haijabainika kutoka kwa utafiti huo iwapo kulala
kwa zaidi ya saa nane huenda ndiko kunakosababisha matatizo hayo ambayo
husababisha kiharusi ama iwapo ni miongoni mwa sababu za magonjwa
yasiojulikana.
Utafiti huo ulifanywa miongoni mwa watu walioko na kati ya
miaka 42 na 81.
Watafiti walichunguza mienendo yao ya kulala kwa kipindi cha
miaka 10 ambapo watu 346 walipatwa na kiharusi.
Baada ya kuangazia athari kama vile miaka na jinsia, watu
waliosema wamekuwa wakilala kwa zaidi ya masaa manane walipatikana na hatari ya
asilimia 46 kupatwa na ugonjwa huo.
Wale walioweza kulala kwa chini ya masaa sita walipatikana
na hatari ya asilimia 18.crdt bbc swahili
No comments:
Post a Comment