Chelsea wametangaza dau kutaka kumsajili mchezaji wa
kimataifa kutoka Japan Yoshinori Muto. Shirika la habari la Japan, Kyodo
limesema mchezaji huyo wa klabu ya FC Tokyo bado hajaamua kama anataka kuhamia
Stamford Bridge au la msimu ujao. Muto, 22, amechezea timu ya taifa mara 11 na
amepachika mabao matatu katika mechi nne za mwanzo wa
msimu mpya wa ligi ya
Japan, J-League. Msimu uliopita alifunga mabao 13 na alitajwa katika kikosi cha
taifa kilichocheza hadi robo fainali ya kombe la Asia. Aliitwa tena na kocha
mpya Vahid Halilhodzic katika mechi yake ya kwanza mwezi uliopita. Muto alifuzu
shahada ya uchumi katika chuo kikuu cha Keio wiki mbili zilizopita. Mwezi
Februari, Chelsea walitangaza mkataba mpya wa udhamini na kampuni ya
kutengeneza matairi ya Japan wenye thamani ya pauni milioni 40 kwa mwaka.
No comments:
Post a Comment