Pages

Friday, April 10, 2015

CHELSEA WAMNYATIA MUTO

Chelsea wametangaza dau kutaka kumsajili mchezaji wa kimataifa kutoka Japan Yoshinori Muto. Shirika la habari la Japan, Kyodo limesema mchezaji huyo wa klabu ya FC Tokyo bado hajaamua kama anataka kuhamia Stamford Bridge au la msimu ujao. Muto, 22, amechezea timu ya taifa mara 11 na amepachika mabao matatu katika mechi nne za mwanzo wa 
 
msimu mpya wa ligi ya Japan, J-League. Msimu uliopita alifunga mabao 13 na alitajwa katika kikosi cha taifa kilichocheza hadi robo fainali ya kombe la Asia. Aliitwa tena na kocha mpya Vahid Halilhodzic katika mechi yake ya kwanza mwezi uliopita. Muto alifuzu shahada ya uchumi katika chuo kikuu cha Keio wiki mbili zilizopita. Mwezi Februari, Chelsea walitangaza mkataba mpya wa udhamini na kampuni ya kutengeneza matairi ya Japan wenye thamani ya pauni milioni 40 kwa mwaka.

No comments:

Post a Comment